Mapishi ya pilau la kuku

Pilau ni mchanganyiko wa mchele na viungo mbalimbali,chakula hiki ni kitamu sana na watu hupendelea sana kupika wakati wa sherehe. Unaweza ukala pilau na kitoweo chochote kile unachopenda mfano mimi nimependa kula na njegere,kachumbali na matunda.

Mahitaji

 • Mchele
 • Kuku
 • Mafuta
 • Vitunguu maji
 • Carrots
 • Pilipili hoho
 • Tangawizi
 • Viungo vya pilau
 • Vitunguu saumu
 • Chumvi
 • Nyanya 3

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Mkate kuku umpike na chumvi akiiva hakikisha supu ya kupikia chakula inatosha.
 • Menya vitunguu maji ukatekate,vitunguu saumu menya utwange na tangawizi,menya carrots uzikwangue na pilipili hoho ukatekate mwisho nyanya pia menya ukate kate.
 • Bandika sufuria utie mafuta, ikichemka tia vitunguu uvikaange. Vikianza kubadilika rangi weka vitunguu saumu na tangawizi mbichi koroga kidoga weka pilipili hoho na carrots.
 • Kaanga kidogo kisha weka nyanya acha ziive na vipande vya kuku koroga kama dk tano weka viungo vya pilau.
 • Weka mchele koroga kisha tia chumvi na umimine supu ile ya kuku kwenye wali.
 • Koroga kisha funika acha chakula chako kiive baada ya dk kumi angalia chakula chako kama maji yamekauka kigeuze palia baada ya dakika kadhaa angalia tena hapo chakula chako kitakua tayari kuliwa.

MAPISHI YAPENDWAYO

Roast ya Samaki
dakika 30
Walaji: 3

Chips za kuoka zenye viungo
dakika 40
Walaji: 2

Wali wa bizari na viungo
dakika 25
Walaji: 2

Toa maoni yakoemwenewa
06:46, Thu 22 May 2014
Naomba recipe za salad aina mbalimbali tafadhali na mbona recipe za kitamaduni kama ugali na mboga mboga na nyinginezo hamuweki?
JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.