Mapishi ya pilipili

Pilipili ni kiungo kinachompa mlaji hamu ya kula chakula,pilipili inaeza kuekwa kwenye chakula chochote mlaji atakapopenda na kufanya mlaji apende chakula chake.

Mahitaji

 • Carrots 3 kubwa
 • Pilipili hoho 1
 • Vitunguu saumu
 • Vitunguu maji 5
 • Tangawizi
 • Majani ya giligiliani
 • Ndimu
 • Chumvi
 • Mafuta kidogo sana
 • Pilipili mbuzi 3 au utakavyopenda
 • Nyanya 3 zilizoiva vizuri

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Menya nyanya,hoho,carrots,vitunguu maji,vitunguu saumu,tangawizi,majani ya giligilian yachambue.
 • Kata kata vitunguu maji na nyanya weka bakuli tofauti,twanga vitunguu saumu na majani ya giligiliani,kwangua carrots pia katakata pilipili hoho.
 • Bandika mafuta jikono yakipata moto weka vitunguu maji koroga dakika 2 weka vitunguu saumu na giligiliani koroga tia tangawizi kisha hoho na carrots.
 • Acha kidogo weka nyanya kamulia ndimu tia chumvi funika mpaka nyanya iive vizuri katia pilipili zako dakika tano baada ya kueka pilipili epua iache ipoe.
 • Ukiona imepoa ieke kwenye blender isage hapo pilipili yako itakua tayari kwa kujiramba.
 • Nahakika utaipenda sana.

MAPISHI YAPENDWAYO

Viazi na nyama ya kusaga
dakika 20
Walaji: 2

Nyama yenye curry sauce
dakika 25
Walaji: 6

Visheti vya vanilla na mdalasini
dakika 15
Walaji: 10

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.