Mapishi ya tambi na kamba

Chakula kinachokupa ladha ya kipekee kutokana na utayarishaji wake. Ni moja kati ya vyakula rahisi bali kwa mapishi haya hakika unapata ladha halisi ya mapishi ya tambi pamoja na mchanganyiko wa viungo tofauti. Ukila chakula hiki utaelewa umuhimu wa kutumia muda kujifunza aina tofauti za mapishi.

Mahitaji

 • Kamba (Prawns) 500g
 • Pilipili manga (Black Pepper) ½ kijiko kikubwa
 • Kitunguu swaumu 1
 • Limao 1
 • Chumvi kijiko kidogo cha chai
 • Curry powder kijiko 1 kikubwa
 • Nyanya 3 (au nyanya za kusaga za kopo)
 • Haradali (Mustard) vijiko 3. (Hii ni maalum kuondoa harufu ya shombo kwenye kamba)
 • Sufuria au kikaango 2
 • Chujio la nazi 1
 • Mwiko 1
 • Sahani 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 Mapishi haya yana hatua tatu muhimu:

 • Kuandaa kamba na kukaanga
 • Kuandaa Tambi
 • Kuchanganya chakula ili kupata mlo kamili.

 Kuandaa kamba

 • Ondoa magamba kwenye kamba kama bado wana magamba

 • Osha kamba kwa kusuuza na maji kiasi.

 • Kamulia limao kwenye kamba, changanya kiasi na kisha ongeza chumvi. Acha kwa muda wa dakika 3, halafu weka hao kamba kwenye chujio ili kuchuja maji na kuacha kama wakavu tayari kwa kupikwa.

 • Bandika kikaango kwenye jiko. Acha ipate moto kiasi, kisha ongeza mafuta ya kula kama ¼ lita (pima kutokana na wingi na ukubwa wa kamba ulionao). Acha yapate moto kwa muda.

 • Ongeza kamba wako kwenye mafuta. Acha waive hadi wabadilike rangi kuanza kuwa wa brauni. Geuza geuza ili waive pande zote.

 • Ongeza haradali kwenye prawns, koroga taratiibu hadi ichanganyike vizuri.

 • Wakishaiva, toa kamba na weka sufuria ya tambi.

Andaa mchuzi wa nyanya

 • Ili kuleta ladha kwenye chakula, andaa mchuzi kiasi wa nyanya na carrot. Kama ulishapika nyama ya mchuzi au kuku ni vizuri kuchukua mchuzi ili kuchanganya na kamba, maana utapata ladha maradufu. Vinginevyo tengeneza mchuzi kiasi wa nyanya ili kuchanganya na kamba.

Andaa Tambi

 • Bandika maji kiasi kwenye sufuria, weka chumvi kisha ongeza tambi.

 • Acha mchanganyiko uchemke kwa muda wa dakika 5 hadi 6. (Angalizo: Tambi huiva chini ya dakika 10, ila itakuwa vizuri kama utatoa wakati bado ngumu ili zisipondeke wakati wa kupika na kamba.)

 • Chuja maji kwenye tambi kwa kutumia chujio.

Changanya 

 • Changanya Tambi kwenye mchuzi wa nyanya. Koroga hadi mchanganyiko uwe vizuri.

 • Changanya kamba kwenye mchanganyiko wa tambi na nyanya. Koroga vizuri. Acha ichemke kwa dakika 3.

 • Ongeza Curry powder na kitunguu swaumu kilichosagwa kwenye mchanganyiko, koroga kiasi.

 • Ongeza pilipili manga kwenye mchanganyiko. Koroga ili kupata mchanganyiko zaidi.

 • Acha mchanganyiko uchemke kwa dakika 2 kisha ipua na unaweza kula.

 • Enjoy.


MAPISHI YAPENDWAYO

Mchemsho wa samaki na ndizi
dakika 20
Walaji: 4

Pilau ya mboga mboga
dakika 35
Walaji: 4

Ndizi mzuzu zilizoiva
dakika 13
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.