Mayai yenye karoti na pilipili hoho

Mayai ni chakula chepesi na chanzo kikubwa cha protini. Unaweza kula chakula hiki muda wowote maana ni rahisi kuandaa na pia kitamu kwa chakula.

Mahitaji

 • Mayai 4
 • Vitunguu 2
 • Karoti 2
 • Pilipili hoho 1
 • Kitunguu saumu punje 2
 • Pilipili manga kijiko 1 kidogo
 • Chumvi

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kuwa huru kuongeza au kupunguza viungo kulingana na unavyopendelea.

misosi-mayai-omelletes-1

 • Andaa kitunguu maji na kitunguu saumu – menya kisha kata vipande vidogo. Osha kisha kata pilipili hoho vipande vya wastani. Menya kisha kata karoti kwenye vipande vidogo. Hifadhi pembeni.
 • Pasua yai, weka chumvi kama unavyopenda, koroga vizuri. Hifadhi pembeni.
 • Bandika kikaango jikoni. Acha kipate moto, kisha weka mafuta ya kula. Yakipata moto, weka kitunguu saumu, kitunguu maji. Koroga vizuri hadi viive. Koroga pamoja, funika acha viive. Baada ya dakika 2 hadi 3, weka pilipili hoho na karoti kisha koroga pamoja. Acha viive kwa dakika 3.
 • Mwagia yai kwenye kikaango, koroga vizuri ili lichanganyike na mboga za majani. Acha liive vizuri upande mmoja, kisha geuza. Unaweza kuvuruga ili kupata vipande vidogo vidogo au unaweza kuacha liungane kama chapati.
 • Geuza upande wa pili, acha kwa dakika 2 kisha epua na weka pembeni. Yai litakuwa tayari kuliwa.
 • Unaweza kula yai hili kwa chakula chochote kile – ugali, wali, au kama kitafunwa chepesi wakati wowote.

misosi-mayai-omelletes-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Pilau la basmati
dakika 35
Walaji: 4

Beef Masala
dakika 15
Walaji: 4

Keki ya chocolate
dakika 55
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.