Mboga ya majani mchanganyiko

Mboga za majani ni muhimu kwa ubora wa afya zetu. Mapishi haya ya leo yanalenga kutoa ujuzi wa kupika aina tofauti za mboga za majani kwa kutumia mboga tulizonazo kila siku majumbani na sokoni. Kumbuka kuwa, kubadilisha aina ya mapishi na uandaaji wa chakula huchangia katika kukupa ladha ya chakula, na kuongeza hamu ya chakula kwako na familia yako pia.

Mahitaji

 • Pilipili hoho 3 – rangi tofauti unazoweza kupata
 • Bamia 6
 • Karoti 2
 • Vitunguu 2
 • Mafuta ya kula (Olive oil ni chaguo zuri)
 • Chumvi

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Leo tunaangalia jinsi ya kuandaa mboga murua ya mchanganyiko ya majani. Mboga yetu itaonekana kama hivi ikikamilika.

20141207_181201

 • Kata kitunguu. Weka kwenye chombo pembeni
 • Kata karoti, tenga pembeni kwenye chombo

20141207_173143

 • Osha bamia, kata na kisha weka kwenye chombo pembeni

20141207_173205

 • Weka sufuria au kikaangio jikoni. Ongeza mafuta na acha yapate moto
 • Weka kitunguu, koroga kiasi. Ongeza bamia, koroga zaidi. Kisha funika kwa muda ili vipate kuiva kwa muda
 • Weka pilipili hoho, koroga ili vipate kuchanganyika
 • Ongea karoti, changanya zaidi

20141207_181159

 • Ongeza chumvi na kisha koroga vizuri ili ipate kuenea vizuri
 • Funika mchanganyiko kwa muda kiasi na mfuniko. Acha ichemke vizuri kwa muda wa dakika 7 hadi 10. Geuza kidogo na kisha funika tena kwa dakika 3 hadi 5.
 • Toa mboga na unaweza kula cha chakula unachopendelea.

20141207_181201


MAPISHI YAPENDWAYO

Kashata za nazi
dakika 12
Walaji: 5

Kashata za nazi
dakika 12
Walaji: 5

Pizza yenye sausage topping
dakika 15
Walaji: 1

Togwa
dakika 30
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.