Mchanganyiko wa mboga za majani

Mchanganyiko wa mboga za majani hizi unakupa virutubisho vyote muhimu unavyohitaji kujenga afya bora. Mie nimeongeza supu ya nyama ili kuupa mchuzi ladha nzuri na virutubisho zaidi. Ni mboga nzuri kula na vyakula kama ugali na wali.

Mahitaji

 • Vitunguu maji 2, menya na kata vipande vidogo
 • Pilipili hoho (Nimetumia 2 za rangi tofauti), menya kata vipande
 • Karoti 2, imenywe na kukatwa vipande vidogo
 • Chumvi
 • Bamia 6, kata ncha, pasua katikati
 • Nyanya chungu 3 – chemsha kwa dakika 5, toa Maganda na hifadhi pembeni.
 • Nyanya 4 (Au tomato paste), menya, kata vipande vidogo au saga ikiwezekana
 • Kitunguu saumu 1, menya, ponda vizuri.
 • Tangawizi 1, imenywe, isagwe vizuri
 • Mafuta ya kula (nimetumia mafuta ya zaituni – olive oil)
 • Unaweza kuwa na sauce ya kuku au nyama ili kuongezea ladha ya hii mboga.

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Ukimaliza kuandaa, mboga itakuwa inaonekana kama hivi:

misosi-mboga-main2

 • Chemsha nyanya chungu kwenye sufuria yenye maji kiasi. Zikiva, menya ngozi ya juu na hifadhi pembeni.
 •  Bandika sufuria au kikaango jikoni, weka mafuta ya kula kiasi. Yakichemka weka kitunguu saumu, koroga. Weka kitunguu maji. Koroga, acha viive na kulainikia kiasi – takribani dakika 3. Weka bamia , ongeza chumvi kiasi. Koroga. Ongeza nyanya, koroga kiasi kisha funika acha ziive vizuri.

Kama ni fresh tomato unaweza kuziponda ili zilainike na kuwa uji baada ya muda, kama ni tomato paste acha ziive vizuri. Hakikisha hazikauki na kuungua, unaweza kuongeza maji kiasi au supu ya nyama ili ziendelee kuiva vizuri.

 • Baada ya dakika kama 8 hadi 10 baada ya nyanya kuchemka, ongeza pilipili hoho na karoti. Koroga vizuri kisha funika.

Mie huwa napenda pilipili hoho zisiive sana, ili nipate virutubisho zaidi na pia harufu nzuri ya pilipili hoho. Kama unapenda ziive vizuri unaweza kuweka mapema ili zikae jikoni muda mrefu, lakini unapunguza virutubisho kwa kuziweka muda mrefu kwenye moto.

 • Sauce ya nyanya ikishaiva weka nyanya chungu. Koroga pamoja vizuri. Kama unatumia supu, huu ndio wakati wa kuchanganya. Koroga vizuri, kisha funika kwa dakika 5 ili supu lichanganyike na chakula.
 • Acha ichemke kwa dakika 3 hadi 5. Epua chakula kitakuwa tayari kuliwa.
 • Hiki mboga inaweza kuliwa pamoja na vitu vingine mfano mkate, chapati, maandazi, au hata wali na ugali. Ni chaguo lako.

misosi-mboga-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Keki ya chocolate
dakika 55
Walaji: 4

Lemonade ya tangawizi
dakika 70
Walaji: 6

Kabeji yenye royco
dakika 10
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.