Mchanganyiko wa mihogo, maharage na samaki kwa kukaanga

Kujiramba ni haki ya kila mmoja. Ukipenda kubadilisha ladha ya misosi kwa kujaribu vitu tofauti, jaribu kula machanganyiko huu mzuri wa vyakula vyenye afya. Ni rahisi kupika na vinakufanya unashiba haswa.

Mahitaji

 • Samaki
 • Kitunguu maji 1
 • Pilipili manga
 • Mihogo (mikubwa) vipande 2
 • Mafuta ya kupikia
 • Cube Maggie
 • Limao/ ndimu/ vinegar
 • Pilipili manga (ya unga)
 • Nyanya 2

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Anza kuandaa samaki. Osha, kwangua magamba na kumkata vipande. Osha na kisha myunyuzie limao (au ndimu au vinegar – ni chaguo lako)
 • Nyunyuzia chumvi, tangawizi, pilipili manga na viungo vingine upendavyo kwenye samaki. Mhifadhi samaki pembeni au kwenye jokofu kwa muda ili viungo viingie vizuri. (kama dakika 15)
 • Menya mihogo, osha na kata vipande vidogo ili iwe rahisi kuiva.
 • Andaa maharage kama ilivyo kwenye maelezo haya (bofya hapa), au kama unaweza kuwa na maharage yaliyo tayari ni vizuri zaidi.
 • Andaa mchuzi wa nyanya. (Unaweza pia kuongeza kipande cha samaki ili kuleta ladha ya samaki kwenye mchuzi)
 • Chemsha mihogo kwenye kikaangio au sufuria hadi iive.
 • Unaweza kuandaa kachumbari ya nyanya, tango na karoti kama unapendelea.
 • Kama mpenzi wa pilipili, usisahau

Tenga chakula chako na ujirambe kwa nafsi yako.


MAPISHI YAPENDWAYO

Mkate wa ndizi na mayai
dakika 75
Walaji: 16

Tambi na mayai
dakika 10
Walaji: 1

Samaki wa ngano na tangawizi
dakika 15
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.