Mchemsho wa samaki na ndizi

Chakula bora chenye virutubisho vyote vya kujenga mwili. Mchemsho kama huu ukila wakati wa mchana ni chakula bora kwa kujenga mwili wako na kuendelea kufanya kazi za kuendeleza maisha.

Mahitaji

 • Samaki 2
 • Ndizi (aina yeyote, katika mapishi haya nimetumia ndizi bukoba)
 • Karoti
 • Pilipili hoho
 • Vitunguu maji
 • Chumvi
 • Nyanya
 • Ndimu

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Menya ndizi na uhifadhi kwenye chombo chenye maji ili zisipate kubadilika rangi
 • Andaa samaki – osha, kata vipande vinavyofaa au kama unapenda mpike mzima – kamulia ndimu. Changanya samaki na limao. Kisha mhifadhi samaki pembeni.
 • Andaa nyanya – osha na kisha menya nyanya 3 na kuzikata vipande vidogo. Hifadhi kwenye chombo.
 • Menya vitunguu maji 2 vikubwa halafu kata kwenye vipande vidogo unavyopendelea.
 • Osha na kisha kata pilipili hoho 1 kubwa kwenye vipande vidogo. Fanya vivyo hivyo kwa carrots 1 kubwa
 • Weka ndizi kwenye sufuria au kikaangio kinachofaa kupikia
 • Weka vitunguu maji juu ya ndizi, halafu weka nyanya juu yake, kisha malizia na karoti.
 • Weka samaki wako kwenye kikaangio kwa kuwapanga vizuri juu ya karoti.
 • Nyunyizia chumvi ya kutosha. Usiongeze mafuta maana kwenye samaki na vitunguu kuna mafuta ya kutosha, hivyo haina haja ya kuongeza zaidi.
 • Weka maji kiasi kama kikombe 1 kikubwa halafu funika na mfuniko usioruhusu mvuke kutoka. Hii inasaidia zile mboga mboga (karoti, pilipili hoho, kitunguu na nyanya) zichuje maji yake na kukipa chakula radha na harufu nzuri.
 • Subiria kwa muda wa dakika 15 hadi 20 na mchemsho wako utakuwa tayari kuliwa.

MAPISHI YAPENDWAYO

Keki ya nanasi
dakika 40
Walaji: 4

Banana muffins
dakika 20
Walaji: 10

Uji wa mchele na ndizi
dakika 35
Walaji: 1

Creamy garlic potato
dakika 40
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.