Mchuzi wa biryani

Sauce hii ya biryani ina ladha tamu kuliwa pamoja na mlo wako wa biryani. Hii sauce ina viambato vingi, unaweza kuweka na kitu chochote kile - nyama, kuku au unachopendelea. Ila kuwa makini, hii sauce ina pilipili hasa, kwahiyo unaweza kupunguza kwa mahitaji yako kama hupendi pilipili.

Mahitaji

 Viungo vingi hapa unaweza kuvipata kwenye maduka ya wahindi.

 Fungu la kwanza

 • Pilipili nyekundu 2, ziwe kavu 
 • Mbegu za giligilani kijiko 1 kikubw
 • Binzari nyembamba ½ kijiko kidog
 • Pilipili manga kijiko 1 kidog
 • Mbegu za mshamari nusu kijiko kidog
 • Mdalasini kiasi
 • Karafuu 3
 • Iliki ya kijani
 • Star anise ua moja

Fungu la pili

 • Vitunguu vidogo 12
 • Pilipili za kijani ndefu 2
 • Kitungu saumu 1
 • Tangawizi kijiko 1 kidogo

Fungu la tatu

 • Majani ya uwatu yaliyosagwa nusu kijiko kidogo
 • Majani ya Bay mawili
 • Pilipili ya unga (kashmiri) kijiko 1 kidogo
 • Unga wa giligilani kijiko 1 kidogo
 • Binzari ya njano robo kijiko kidogo
 • Majani ya giligilani vijiko viwili vya chakula yakatekate
 • Mafuta vijiko 3 vya chakula
 • Nyanya 2 zilizoiva vizuri
 • Tui zito la nazi kijiko 1 kidogo
 • Chumvi kijiko 1 na nusu kidogo
 • Maji nusu kikombe kama utatumia
 • Majani ya binzari matano

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Changanya viungo vyote vya fungu la kwanza pamoja kisha weka kwenye mashine ya kusagia viungo. Saga hadi viwe unga laini. Viache kwenye chombo cha kusagia.
 • Menya viungo vya fungu la pili – vitunguu, pilipili, kitunguu saumu na tangawizi – kisha kata kwenye vipande vidogo
 • Changanya viungo vya fungu la pili kwenye chombo cha kusagia. Endelea kusaga kwa pamoja. Usiweke maji hata kidogo. Vikishasagika vizuri, toa weka pembeni.
 • Bandika kikaango chenye mafuta ya kula jikoni. Weka majani ya bay, uwatu na majani ya binzari. Pika kama dadika 2, kisha weka mchangantiko wa vitunguu kwenye sufuria. Koroga vizuri halafu punguza moto uwe wa wastani. Pika kwa dakika 12
 • Weka nyanya, pilipili ya unga, giligilani, binzari na chumvi. Koroga vizuri. Pika kwa dakika 10, usiache kukoroga hadi mafuta yajitenge na mchuzi uwe rangi ya udongo (brown)
 • Kwenye hatua hii unaweza kuongeza chochote – kuku, nyama au mboga mboga. Ukishaweka unachotaka, ongeza maji kidogo. Funika na acha mboga yako iive vizuri
 • Mwisho weka tui la nazi. Acha lichemke kwa dakika 5 kisha katia majani ya giligilani juu yake
 • Epua. Tenga na biryani, acha watu wajirambe.

MAPISHI YAPENDWAYO

Mapishi ya tambi na kamba
dakika 20
Walaji: 2

Maandazi ya Mayai na Maziwa
dakika 20
Walaji: 4

Samaki wa kupaka
dakika 25
Walaji: 2

Tambi za hiliki na sukari
dakika 8
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.