Meat loaf

Meat loaf ni chakula kizuri na rahisi kuandaa. Chakula hiki ni kitamu unaweza kula kwa aina yoyote ya kinywaji pia waweza kula muda wowote iwe asubuhi, mchana au usiku na familia ikakifurahia.

Mahitaji

 • Butter vijiko 3
 • Vitunguu maji 3
 • Figili fungu 1
 • Carrot 2
 • Vitunguu saumu 2
 • Chumvi vijiko 2 vya chai
 • Pilipili manga kijiko 1 cha chai
 • Nyama ya kusaga kilo 2 inaweza ikawa ya ng'ombe, kondoo au yoyote
 • Majani ya parsley
 • Mayai 2
 • Worcestershire sause vijiko 2
 • Thyme
 • Mkate ila toa ganda gumu la pembeni
 • Vitunguu vya majani
 • Maziwa robo lita
 • Ketchup

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Bandika sufuria weka butter acha iyeyuke. Kisha weka vitunguu maji, carrot na figili, pika mpaka vilainike kisha punguza moto, weka vitunguu saumu na katia na vitunguu vya majani, pika kwa sekunde 30.
 • Ongeza viungo vinaitwa thyme na nyanya ya kopo koroga mpaka uhakikishe vimeiva epua.
 • Chukua bakuli kubwa, weka nyama, mayai,worcestershire sause, chumvi, pilipili manga, mkate, maziwa na zile mboga ulizopika.
 • Changanya vizuri ila tumia mikono kuchanganya mpaka vichanganyike vizuri, na uhakikishe viungo vimeshika vizuri kwenye huo mchanganyiko.
 • Weka mchanganyiko kwenye chombo utakachotumia kuokea, ni vizuri ukatumia chombo cha kuokea mkate.
 • Mwagia ketchup kwa juu ya mchanganyiko, sambaza kwa juu mpaka ienee vizuri kisha oka.
 • Oka kwa dakika 45 kisha itoe meat loaf mwagia tena ketchup kwa juu na uisambaze. Rudisha tena kwenye oven kwa dakika 15, epua iache ipoe.
 • Iache kama dakika 10, katakata slice tenga watu wajirambe.

MAPISHI YAPENDWAYO

Kuku wa limao
dakika 45
Walaji: 4

Mkate wa kuku na mayai yake
dakika 40
Walaji: 4

Viazi vya mboga mboga
dakika 18
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.