Mexican sauce na chapati za maji

Unapenda kujaribu vitu tofauti? Haya ni mapishi matamu ya mexican sauce. Ni kuku au nyama unayoweza kupika kwa aina tofauti. Viungo vya mapishi haya huleta ladha na harufu nzuri na kukufanya upate utamu na raha ya kujiramba na huu msosi.

Mahitaji

 

 • Minofu ya kuku ¼ kilo
 • Indian Curry
 • Cube Maggie
 • Limao au ndimu
 • Tangawizi
 • Pilipili manga
 • Pilipili hoho
 • Kitunguu kikubwa 1
 • Mafuta ya kula
 • Wraps au chapati za maji.

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Anza kuandaa nyama. Kata vipande vidogo na vyemamba sana ili iwe rahisi kuiva. Osha na kisha nyunyuzia limao. Weka chumvi, tangawizi na kitunguu saumu. Chanyanya mchanganyiko. Acha ikae kwa dakika kama 15 ili viungo vipate kuingia vizuri.
 • Andaa pilipili hoho, kitunguu maji na karoti. Osha kisha kata kwa urefu, upate vipende virefu ambavyo vitapendeza kuchanganya kwenye nyama.
 • Bandika kikaangio au sufuria jikoni na weka mafuta ya kula ya kutosha. Acha yapate moto vizuri.
 • Weka nyama ya kuku, koroga kiasi na kisha acha ikaangike vizuri. Subiria hadi nyama ipate kubadilika rangi na kuwa ya brown.
 • Weka mboga za majani – pilipili hoho, kitunguu, na karoti. Funika kwa muda ili vipate kuiva na mvuke.
 • Weka curry kiasi, kisha koroga. Ni vizuri kama nyama itaanza kuwa na rangi ya curry.
 • Weka tangawizi kiasi, koroga na acha kwa dakika 1
 • Weka pilipili manga ya unga, na kisha koroga vizuri.
 • Weka cube maggie na kisha koroga.
 • Acha mchanganyiko kwa muda wa dakika 3 hadi 5 ili uive vizuri. Kisha ipua chakula.

Andaa chapati zako (au mexican wraps) na kisha weka nyama juu yake. Hapa chakula kinakuwa tayari kula. Jirambe na uhondo wa mexican sauce.

mexican--misosi2

misosi-mexican


MAPISHI YAPENDWAYO

Maandazi ya apple
dakika 5
Walaji: 5

Tambi za maziwa na iliki
dakika 15
Walaji: 3

Nyama ya kukaanga
dakika 30
Walaji: 3

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.