Mille feuille pastry

Keki ya Millefeuille ni kitafunwa pendwa na rahisi kuandaa cha kifaransa, wengine hukita Napoleon, ni mfano wa keki maarufu sana kwenye jamii ya kifaransa ambayo huliwa kama dessert, au kitindamlo. Keki hii inatengenezwa kwa matabaka tofauti ya mfano wa biskuti (unga uliookwa kwa kutumia siagni) pamoja na viambato vingine tofauti. Hii keki yetu tumeiandaa kwa kutumia vanilla cream na cocoa. Ni keki tamu na rahisi sana kuandaa. Wape raha wale uwapendao.

Mahitaji

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Mapishi haya yametumia unga uliochanganywa kwa siagi kama ilivyoelezwa hapa. Ni muhimu kufuata maelekezo haya ili kupata matokeo mazuri zaidi. Pia unaweza kuongeza au kupunguza mahitaji kulingana na unavyopendelea.

millefeuille000

 • Washa oven kwenye nyuzijoto 392°F (200°C). Acha ipate moto wakati unaendelea na maandalizi.
 • Kwenye sinia la kuokea kwenye oven, tandaza karatasi inayoweza kutumika kuokea, paka mafuta ya kula juu yake kwa kutumia brush kisha tandaza dida la unga (unga wa ngano uliochanganywa na siagi). Paka maji juu ya dida la unga kwa kutumia brush, hakikisha yameenea vizuri. Nyunyizia kijiko 1 cha sukari juu ya dida la unga kisha funika na karatasi lingine linaloweza kutumika kwenye oven. Juu yake weka sinia lingine la kuokea. Weka kwenye oven.
 • Oka kwa dakika 15 kisha toa kwenye oven. Toa sinia na karatasi la juu, dida litakuwa limegeuka kama biskuti, geuza upande wa pili kisha tandaza sukari juu yake. Funika na karatani na sinia la kuokea kama mwanzo, rudisha kwenye oven kwa dakika nyingine 10.
 • Toa pande kubwa la biskuti iliyoiva na weka kwenye ubao wa kukatia. Kuwa makini ni gumu hivyo linaweza kukatika kirahisi. Kata biskuti kwenye  vipande vitatu vinavyolingana ukubwa.

millefeuille006

 • Tandaza nusu ya vanilla cream nusu ya juu ya biskuti mojawapo kisha tandaza ili ienee biskuti nzima. Safisha pembezoni mwa pande la biskuti kwa kutumia kisu, toa upukupuku wa biskuti unaomwagika. Weka kipande cha pili cha biskuti juu ya kile kilicho na vanilla cream. Unaweza kukikata kwenye vipande vidogo au ukakiweka kikiwa kizima, ni chaguo lako.

millefeuille005

 • Weka cream ya vanilla iliyobaki juu ya kipande cha biskuti na  tandaza hadi iendee biskuti nzima. Weka kipande cha tatu juu yake, hakikisha vimewiana vizuri ili iwe rahisi kukata. Unaweza kukikata kwenye vipande vidogo au ukakiweka kikiwa kizima, ni chaguo lako.

millefeuille003

millefeuille004

 • Kwenye bakuli, changanya icing sugar na kijiko 1 cha maji. Koroga vizuri hadi iwe laini. Kwenye bakuli tofauti, changanya cocoa na maji, koroga pamoja hadi iwe laini. Weka cocoa kwenye mfuko wa plastiki na toboa tundu dogo ili uweze kuiminya vizuri wakati wa kuimimina juu ya icing sugar.
 • Tandaza mchanganyiko wa icing sugar juu ya biskuti ya tatu ya millefeuille. Hakikisha unafanya hii kwa haraka ili icing sugar isigande wakati unaendelea na zoezi la kumalizia kuandaa keki. 

millefeuille008

 • Mwaga cocoa kwenye mistari kama 5 ya cocoa ikifuatana na upana wa keki. 

millefeuille002

 • Tandaza Cocoa kwa kutumia kijiti kupata maumbo unayopendelea

millefeuille001

 • Kata vipande vidogo vidogo ili iwe rahisi kugawa na kula. 

millefeuille000

 • Ukimaliza, hifadhi keki sehemu ya ubaridi ili icing sugar ipate kuganda kabla ya kuila. Baada ya dakika 30 unaweza kujiramba na keki hii ya Millefeuille.

mille-feuille-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Chips mayai na mboga za majani
dakika 20
Walaji: 2

Mishikaki ya kupaka
dakika 30
Walaji: 4

Ugali wa muhogo na mlenda
dakika 15
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.