Mishikaki ya kupaka

Mishikaki ni chakula kitokanacho na nyama ya mbuzi, samaki, kuku au nyama nyingine yoyote. Mishikaki ya kupika kwa kutumia viungo mbalimbali inayoweza kuliwa wakati wa chakula au kama kitafunwa na kinywaji. Utamu wake unaletwa na mchanganyiko adhimu wa viungo. Ni murua kutumia kwa kujiliwaza pamoja na familia au marafiki. Jirambe...

Mahitaji

 • Nyama kilo 1
 • Mafuta ya olive vijiko 3 vya chakula kwa ajili ya kulowekea
 • Kitunguu saumu
 • Tangawizi iliyosagwa vijiko 3
 • Pilipili manga
 • Papai bichi
 • Siki nyeupe vijiko 2
 • Chumvi
 • Binzari kijiko 1
 • Majani ya giligiliani kijiko 1
 • Mdalasini kijiko 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Kata nyama vipande vikubwa kisha osha mara moja tu.
 • Weka viungo kwenye nyama - kitunguu saumu, tangawizi, pilipili manga, papai bichi, mdalasini, binzari, siki, giligiliani, chumvi. Changanya vizuri viungo viingie vizuri kwenye nyama.
 • Viungo vikishachanganyika vizuri mimina mafuta kwenye nyama. Mafuta haya ni kwa ajili ya kulowekea nyama.
 • Weka nyama  kwenye fridge kwa muda wa masaa mawili ili viungo vishike vizuri.
 • Baada ya masaa mawili, anza kutunga nyama kwenye miti ya kuchomea tayari kwa kuchoma
 • Ni vizuri kuchoma mshikaki kwa kutumia jiko la mkaa lakini unaweza kutumia jiko lolote lile - oven au nishati yoyote unayopendelea. Cha msingi hakikisha moto uwe wa wastani ili nyama iive vizuri.
  Kitu cha kuzingatia hapa ni kuwa, nyama inatakiwa kuiva vizuri nje na ndani. Moto mkali utababua nyama kwa nje na kuzuia kuiva vizuri ndani. Kama unatumia jiko la mkaa ni vizuri kugeuza mara kwa mara ili nyama ipate kuiva vizuri pande zote. Kama unatumia Oven huna haja ya kugeuza maana ni rahisi joto kuingia kwa uwiano mzuri kwenye nyama.
 • Choma nyama kwa kugeuza geuza mpaka mishikaki iive vizuri.
 • Jirambe.

MAPISHI YAPENDWAYO

Pilau la basmati
dakika 35
Walaji: 4

Beef Masala
dakika 15
Walaji: 4

Keki ya chocolate
dakika 55
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.