Mishikaki mitamu yenye papai

Mishikaki huwa ni mitamu, je umeshajaribu mishikaki ya papai? Hii ni mishikaki inayokupa ladha zaidi kutokana na uwepo wa papai, bizari na pilipili. Nyama huwa laini, yenye harufu nzuri na kuvutia. Hii haiishii machoni tu, bali mdomoni unapata ladha zaidi kwa kuchangamsha vionjo vya ulimi.

Mahitaji

 • Nyama steki kilo 1, kata vipande vya mraba kisha osha vizuri
 • Tangawizi kijiko 1 cha chakula
 • Kitunguu saumu kijiko 1 cha chakula
 • Papai bichi vijiko 3 vya chakula
 • Chumvi vijiko 2 vya chai
 • Pilipili ya unga nyekundu kijiko 1 cha chai
 • Bizari kijiko 1 cha chai
 • Mafuta ya kupikia vijiko 2 vya chakula
 • Nyanya paste kijiko 1 cha chakula
 • Limao kijiko 1 cha chakula
 • Curry powder kijiko 1 cha chakula

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Ni vizuri kuandaa nyama mapema, ukiweka na viungo ili ipate kulainika vizuri kabla ya muda wa kupika. Kula mishikaki ikiwa ya moto na imeiva vizuri, hii itakufanya upate raha zaidi.

 • Kwenye sufuria au bakuli, weka viungo vyote kisha changanya pamoja hadi viungo vichanganyikane vizuri.
 • Weka nyama kwenye mchanganyiko wa viungo kisha funika, weka kwenye jokofu kwa usiku mzima ili ilainike na iwe na ladha tamu. Muda mrefu nyama ikikaa na viungo huifanya izidi kulainika na kuongea utamu.
 • Ikifika muda wa maandalizi, tunga nyama kwenye vijiti vya mishikaki kisha weka juu ya wavu uliopakwa mafuta. Waweza tumia jiko la mkaa au oven kuandaa mishikaki yako. Choma nyama huku ukiilanisha kwa mafuta kadri unavyoendelea kuichoma ili nyama isiwe kavu.

Kama unatumia oven, unaweza kupaka mishikaki mafuta mapema ili ipate kuiva taratibu na kupunguza muda wa kutoa na kupaka mafuta. Ni vizuri kutumia mafuta yenye afya, kama mafuta ya zaituni.

 • Endelea kugeuza nyama  wakati wa kuchoma mpaka iive na kua laini. Zingatia kutoiacha nyama kwa muda mrefu kwenye moto kuepuka kukauka na ngumu.
 • Epua, tenga na jirambe. Usisahau vionjo vitamu vya kulia pamoja na mishikaki.

mishikaki-papai-main2


MAPISHI YAPENDWAYO

Kachori tamu zenye giligilani
dakika 20
Walaji: 6

Keki tamu ya mtindi na vanilla
dakika 50
Walaji: 8

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.