Mishikaki ya kupaka

Mapishi ya mishikaki yanayokuliwaza na kukupa raha ya maisha. Ni rahisi kuandaa, inafaa kuliwa vizuri taratibu ukiwa umepumzika nyumbani wakati unapata kinywaji cha kukupa afya na familia.

Mahitaji

 • Nyama kilo 2 ikiwa kwenye vipande vidogo vidogo
 • Nyanya 1 – menya na kata vipande
 • Tangawizi 1 kata vipande vidogo
 • Kijiko 1 cha cumin ya kusaga
 • Karafuu 4
 • Limao 1
 • Mafuta ya kula kijiko 1
 • Kiwi 1 – Menya na kata vipande. Inasidia kulainisha nyama
 • Coriander 1/2 kikombe
 • Pilipili mbuzi 2
 • Kijiko 1 cha paprika
 • Bizari ½ kijiko
 • Chumvi

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Changanya kila kitu, kasoro nyama, kwenye blender na kisha saga vizuri
 • Chovya nyama vizuri ili ipate kulowa vizuri.
 • Weka nyama iliyochovywa kwenye jokofu usiku mzima ili kupata matokeo mazuri zaidi
 • Choma nyama kwenye jiko la mkaa, ili kupata ladha halisi.
 • Unaweza kuchanganya mishikaki kama utakavyo, ila ni vizuri kama utaweka pilipili hoho na karoti ili kuipa mishkaki muonekano mzuri na kuongeza utamu.
 • Unaweza kula na mkate au kitafunwa chochote kinachokufurahisha kutafuna na mishkaki.

MAPISHI YAPENDWAYO

sweet and sour chicken
dakika 25
Walaji: 2

Caramel cheese cake
dakika 60
Walaji: 5

Mkate wa zucchini na korosho
dakika 55
Walaji: 5

Keki ya nanasi
dakika 40
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.