Mishikaki ya ng'ombe kwa kuoka kwenye oven

Weekend huwa muda mzuri sana kwangu kujaribu vitu vingi, maana napata wakati wa kutosha wa kufanya mambo mengi. Weekend hii nilijaribu kuandaa mishikaki ya ng’ombe kwa kutumia oven. Sikuwa najua matokeo yatakuwaje lakini ikatokea vizuri. Kujaribu siyo vibaya, maana ndio mwanzo wa kujifunza. Unaweza pia kujaribu, mie nimefurahia sana maana niliweka sauce iliyo na viungo vingi na imefanya nyama imekuwa tamu.

Mahitaji

Kwa nyama

 • Chumvi
 • Tangawizi
 • Nyama ½ kilo (Vizuri kama itakuwa steki)
 • Pilipili hoho 2 (Kijani na nyekundu)
 • Miti ya mishikaki

Kwa sauce ya kulowekea nyama (marinade)

 • Kitunguu saumu 1, kimenywe na kupondwa vizuri. Au tumia cha unga.
 • Limao 1
 • Tandoori (Hii inapatikana sana kwenye maduka yauzayo viungo vya chakula vya kihindi)
 • Maggi cube
 • Sweet pepper au capsicum (Ni pilipili kama hoho maana haina ukali, na ni unga unga, utapata kwenye maduka yanayouza viungo vya chakula zaidi kwa wahindi)
 • Mafuta ya kula vijiko 2 vikubwa (Nimetumia olive oil)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Ukimaliza kuandaa mishikaki yako itakuwa hivi:

misosi-mishikaki-oven

Andaa sauce ya kuloweka nyama (Marinade):

 • Changanya kila kitu pamoja – kitunguu saumu, sweet pepper, tandoori, maggi cube na mafuta ya kula. Kata limao kisha kamulia. Kwenye mchanganyiko. Koroga pamoja hadi ichanganyike vizuri kabisa.  Hifadhi pembeni.

misosi-mishikaki-marinade

Andaa nyama:

 • Kata nyama kwenye vipande vya wastani, visiwe vidogo sana maana vitaungua. Osha na kisha hifadhi pembeni.
 • Kata pilipili hoho, karoti vipade vyenye ukubwa wa wastani.

misosi-mishikaki5

 • Anza kutunga mishikaki kwa kuweka nyama na mboga mboga pamoja.

misosi-mishikaki6

 • Mwagia sauce juu ya mishikaki iliyo tayari. Paka vizuri hadi sauce iingie kila sehemu. Hifadhi kwenye chombo safi na weka kwenye jokofu (fridge) kwa muda wa masaa mawili ili vipate kuchanganyika.

misosi-mishikaki7

 • Muda ukifika, washa oven kwenye nyuzijoto 350°F (185°C) kwa dakika 10. Kisha weka mishikaki kwenye waya wa oven. Geuza mara kwa mara ili mishikaki isiungue. Baada ya dakika 30 hadi 40 itakuwa tayari.
 • Jirambe na mishikaki mitamu.

misosi-mishikaki2

misosi-mishikaki-oven

 


Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.