Mkate wa boga

Mahitaji

 •  Vikombe 3 vya boga lililosagwa 
 •  Mafuta kikombe 1 na nusu
 •  Vikombe 4 vya sukari nyeupe
 •  Mayai 6
 •  Unga vikombe 4 na robo tatu
 •  Baking powder kijiko 1 na nusu cha chai
 •  Baking soda kijiko 1 na nusu cha chai
 •  Chumvi kijiko 1 na nusu cha chai
 •  Mdalasini kijiko 1 na nusu cha chai
 •  Nutmeg kijiko 1 na nusu cha chai
 •  Karafuu kijiko 1 na nusu

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Washa oven kwenye nyuzijoto 350°F (176°C) wakati unaandaa mahitaji.
 • Paka mafuta chombo utakachotumia kuoka mkate kisha nyunyiza unga juu yake. Paka unga uenee vizuri kuzunguka chombo chote. Unga utakaozidi toa.
 • Kwenye bakuli kubwa, pasua mayai kisha koroga vizuri. Weka boga, mafuta na sukari. Changanya kwa pamoja vizuri.
 • Kwenye bakuli tofauti – weka unga, baking soda, baking powder, chumvi, mdalasini, nutmeg na karafuu. Changanya vizuri.
 • Changanya mchanganyiko wa unga ule wa mayai pamoja. Changanya vizuri hadi uwe na uzito wa wastani.
 • Weka walnuts, changanya. Weka mchanganyiko kwenye chombo cha kuokea.   Weka kwenye oven, tega muda wa saa 1. Muda ukifika, angalia kama imeiva, kisha tena na ujirambe.

MAPISHI YAPENDWAYO

Mapishi ya spinach
dakika 18
Walaji: 3

Mapishi ya pilau la kuku
dakika 25
Walaji: 5

Mapishi ya pilipili
dakika 15
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.