Mkate wa chocolate na strawberry

Kuandaa vitu vitamu, hasa kuoka mikate, cake, maandazi na vingine ni wakati murua sana kupitisha muda wangu. Niliwahi kuonja huu mkate kabla ya kuuandaa, na sikuweza kujizuia, ikabidi niandae tu ili nipate kuhisi tena ile ladha tamu. Hakika familia ilifurahia na tulijiramba hasa. Ni mkate ulio bora, rahisi kuandaa na hauhitaji ujuzi mkubwa sana, bali ni mapenzi yako na muda mchache sana. Jirambe na mkate wa chocolate na strawberry.

Mahitaji

 • Kikombe 1 cha strawberry (zilizokatwa vipande vidogo vidogo)
 • Sukari  ¾ kikombe (nimetumia sukari ya brown)
 • Unga wa ngano Kikombe 1 ½
 • Mafuta ya kula ½ kikombe
 • Mayai 2
 • Vipande vya chocolate ½ kikombe
 • Mdalasini Kijiko 1½
 • Chumvi ½ kijiko
 • baking soda ½ kijiko

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Leo tunaandaa mkate mtamu sana ulio na strawberry na chocolate. Haya mapishi yalishawahi kuwekwa hapa, yana maelezo yenye picha.

chocolate-bread-main

 • Kama unatumia oven, washa kwenye nyuzi joto 320°F (au 180°C) ili ipate moto wakati unandaa mchanganyiko wa mkate.
 • Changanya sukari, unga, mdalasini,  chumvi na baking soda kwenye bakuli kubwa na koroga vizuri.
 • Kwenye bakuli tofauti, weka mafuta ya kula, pasulia yai juu yake na koroga vizuri hadi vipate kuungana sawia.
 • Ongeza vipande vya chocolate na strawberry kwenye bakuli yenye mchanganyiko wa mafuta na chocolate. Koroga vizuri ili vichanganyike.
 • Minipa rojo la mafuta na mayai kwenye unga. Koroga vizuri hadi lilainike vizuri.
 • Mimina mchanganyiko wako kwenye bakuli unalotumia kuoka kwenye oven. Weka bakuli kwenye oven, tega dakika 45 ili ipate kuiva.
 • Kama unatumia rice cooker, mimina mchanganyiko kwenye bakuli la rice cooker, kisha washa na tega saa 1 (kama linaruhusu) au likizima kabla ya muda endelea kuliwasha hadi muda wa saa 1 ufikie.
 • Baada ya dakika 45  (au saa 1 kama unatumia rice cooker) tumbukiza toothpick (kijiti kisafi cha kuchokonolea meno au njiti ya kiberiti) ili kuona kama mkate umeiva. Kikitoka kikavu, mkate umeiva, vinginevyo rudisha tena kwa dakika 5 hadi 10 ili upate kuiva.
 • Unaweza kula mkate huu ukiwa wa moto au baridi, utamu uko pale pale.

chocolate_chip_strawberry_b


MAPISHI YAPENDWAYO

Pound cake
dakika 60
Walaji: 4

Salad ya kabichi
dakika 5
Walaji: 5

Mtori wa ndizi
dakika 45
Walaji: 1

Pilipili ya maembe ya kusaga
dakika 35
Walaji: 5

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.