Mkate wa kiwavi wenye kuku

Mkate huu umetengenezwa kwa umbo la kiwavi ili kukupa hamu zaidi ya kuula. Utengenezaji wake unahitaji mbinu chache na rahisi sana, ila matokeo yake ni mazuri na mkate unakuwa mtamu kutokana na viungo vinavyotumika. Huu mkate nimeufurahia maana ulikuwa unanipa hamu ya kuula kupita kiasi, na utamu wake umedhihirika pia. Nakupa na wewe ujionjee ili upate kula vitamu kama mie.

Mahitaji

Kuandaa mkate huu tutakuwa na mahitaji ya aina mbili tofauti.

Mahitaji kwa Unga wa mkate

 • Unga wa ngano, kilo 1
 • Maziwa ya unga vijiko 2 vikubwa
 • Hamira kijiko 1 cha chai
 • Mayai 2 (Moja la kuchanganya kwenye mkate, lingine utapaka mwisho)
 • Vijiko 4 vikubwa vya mafuta ya kula
 • Sukari laini (Au unaweza kuisaga)
 • Chumvi kijiko 1 cha chai
 • Ladha ya Vanilla (Vanilla flavour)
 • Ufuta (kidogo tu wa kunyunyizia kwenye mkate)
 • Maji ya moto ¼ lita (kwa kukandia)

Mahitaji kwa kutengeneza sauce ya kuku

Sauce ya kuku ilishaandaliwa na mkate wa kusuka uliwekwa hapa.

 • Minofu ya kuku ¼ kilo
 • Kitunguu 1 kilichokatwa vipande vidogo
 • Majani ya Korianda
 • Kijiko 1 cha chai
 • Pilipili ndogo za kijani, zikate vipande vidogo
 • Masala Kijiko 1 cha chai
 • Pilipili manga
 • Unga vijiko 2 vikubwa
 • Kikombe 1 cha maziwa

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Mie binafsi nimefurahia sana mkate huu, maana una kila aina ya utamu na virutubisho. Ukimaliza kupika, utakuwa na mkate unaoonekana hivi:

caterpillar-bread-recipe1

Katika kuandaa mkate wetu, tutaandaa katika hatua kuu 2. 

1. Kuandaa nyama ya kujazia kwenye mkate

Unaweza kutumia kitu chochote kujazia ndani ya mkate. Mfano : sausage, mboga za majani, viazi nk. Ila kama unataka kuandaa nyama hii ya kuku, unaweza kuangaia kwa urefu hapa. Cha muhimu kabla hujaanza kuandaa, hakikisha kuku amechemshwa vizuri na amepondwa vizuri. Kwa ufupi, haya hapa maelezo yake.

 • Bandika kikaango, weka mafuta. Acha yapate moto.
 • Weka kitunguu. Koroga hadi kigeuke rangi na kiwe laini.
 • Weka unga, chumvi, pilipili manga, na masala. Koroga pamoja kama dakika 2 hadi 3.
 • Weka maziwa, koroga vizuri. Acha iive kiasi hadi iwe uji mzito.
 • Weka pilipili za kijani, ongeza majani ya korianda. Koroga vizuri.
 • Weka kuku. Koroga vizuri.
 • Bandua toka jikoni. Hifadhi pembeni acha ipoe.

20150117_141145

2. Kuandaa mikate

Tafadhali soma maelezo ya kutayarisha unga kabla ya kufika hatua hii kwenye ukurasa huu wa mkate wa kusuka au ukurasa huu unaohusu kuandaa unga na kukanda.

 • Kabla ya kuendelea, hakikisha umeshakanda unga na kuuacha uumuke kwa muda. Pata maelezo zaidi kwa kusoma hapa jinsi ya kuandaa unga na kukanda.
 • Washa oven, weka nyuzijoto 180°C.
 • Tandaza unga mkavu kiasi kwenye meza au ubao unaotumia kukandia.
 • Weka unga uliokandwa kwenye meza ya kukandia, kisha kanda tena ngano yako kidogo. Hii inasaidia kuondoa hewa iliyobaki ndani ya unga.

20150118_162000

 • Gawa ngano kwenye mabonge machache kulingana na idadi ya mikate unayotaka.
 • Anza kutengeneza shepu unazotaka za mkate. Tafadhali angalia picha hapo chini.
 • Changanya nyama ya kuku uliyoandaa. Weka kwenye mkate kisha funga vizuri.
 • Ukimaliza kufunga, pasua yai, koroga na changanya maji kidogo. Paka mchanganyiko wa yai juu ya mkate kisha mwagia ufuta.
 • Panga mikate kwenye chombo cha kuokea
 • Weka mikate kwenye oven. Acha iive kwa muda wa dakika 30 hadi 40.
 • Angalia mikate kama imeiva.

catepillar2

Maelezo ya picha

1. Baada ya kukanda, tenga mabonge ya mkate kutokana na idadi ya mikate unayotaka kuandaa

2. Tandaza vizuri kwenye sehemu ya kukandia. Weka nyama ya kujazia, juu ya unga wako ulioutandaza vizuri.

3. Kata ngano yako kwa kisu vizuri mistari karibu karibu ili kuweza kutengeneza umbo unalotaka

4. Anza kukunja ngano yako. Kunja kuanzia kwenye nyama na kuizungusha hadi kufikia mwisho kule ulipochana

5. Ukishamaliza, paka majarini (siagi) na mwagia mchanganyiko wa yai na maji (egg wash) ili kuongeza ladha kwenye mkate wako. Hii ndio inanogesha zaidi. Kisha weka kwenye oven kwa muda wa dakika 30 hadi 40.

6. Mkate wako tayari kuliwa, jirambe

Jirambe


MAPISHI YAPENDWAYO

Dagaa wa nazi na karanga
dakika 15
Walaji: 4

Sausage Stroganoff
dakika 10
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.