Mkate wa kuku na mayai yake

Mkate wa kuku na mayai ni kitafunwa kitamu sana na vizuri kuandaa nyumbani. Ni mkate unaotakiwa kuandaliwa wa mapenzi na upendo wote ili kuupa ladha na utamu unaotakiwa. Angalia jinsi ya kuandaa mkate huu kwa picha zilizoonyeshwa vizuri kwenye maelezo haya.

Mahitaji

1. Mahitaji kwa Unga wa mkate

 • Unga wa ngano, ¾ kilo
 • Maziwa ya unga vijiko 2 vikubwa
 • Hamira kijiko 1 cha chai
 • Mayai 2 (Moja la kuchanganya kwenye mkate, lingine utapaka mwisho)
 • Vijiko 4 vikubwa vya mafuta
 • Sukari laini (Au unaweza kuisaga)
 • Chumvi kijiko 1 cha chai
 • Ladha ya Vanilla (Vanilla flavour)
 • Ufuta
 • Maji ya moto ¼ lita

2. Mahitaji kwa kutengeneza sauce ya kuku

 • Minofu ya kuku ¼ kilo
 • Kitunguu 1 kilichokatwa vipande vidogo
 • Majani ya Korianda
 • Kijiko 1 cha chai
 • Pilipili ndogo za kijani, zikate vipande vidogo
 • Masala Kijiko 1 cha chai
 • Pilipili manga
 • Unga vijiko 2 vikubwa
 • Kikombe 1 cha maziwa

 

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kwenye mapishi haya ni vizuri kama utatumia vipimo maalum. Ingawa unaweza kuendelea na vipimo vya kawaida, ila ladha itatofautiana sana kama usipotumia vipimo maalum ili uweze kutengeneza mkate ulio sawa na huu. Ukishafanya mara ya kwanza, unaweza kujaribu unavyopenda baadae, maana mapishi ni utundu wako tu.

Maelezo haya yanaweza kuonekana marefu kwa wale wazoefu na wajuzi, lakini nimeweka hivi makusudi kusaidia wale wasiojua kuandaa unga hadi kufika wakati wa kukanda. Kama mzoefu, unaweza kuruka hatua ya 2, maana inaelezea jinsi ya kukanda unga.

1. Kuandaa nyama ya kujazia kwenye mkate

Mkate wetu tunaujaza nyama kwa ndani, ndio maana tunaika mkate wa nyama ya kuku. Muhimu ni kuhakikisha kuku amechemshwa vizuri na amepondwa vizuri. Unaweza pia kupata maelezo ya kuandaa nyama hii kwa urefu hapa.

 • Bandika kikaango, weka mafuta. Acha yapate moto.
 • Weka kitunguu. Koroga hadi kigeuke rangi na kiwe laini.
 • Weka unga, chumvi, pilipili manga, na masala. Koroga pamoja kama dakika 2 hadi 3.
 • Weka maziwa, koroga vizuri. Acha iive kiasi hadi iwe uji mzito.
 • Weka pilipili za kijani, ongeza majani ya korianda. Koroga vizuri.
 • Weka kuku. Koroga vizuri.
 • Bandua toka jikoni. Hifadhi pembeni acha ipoe.

 

20150117_141230

2. Kuandaa unga 

Unaweza kuruka hatua hii kama ni mzoefu wa kukanda unga, unaweza kuruka hatua hizi na kuanza kwenye kuchanganya na kupika.

 • Weka maji kwenye bakuli (iwe ya udongo au plastiki, isiwe ya bati au chuma)
 • Ongeza sukari (Unaweza pia kuweka asali vitone kidogo sana). Koroga vizuri ili vichanganyike.
 • Mwagia hamira. Tafadhali usikoroge. Mwaga juu ya maji kwenye bakuli na funika na kitambaa kwa muda wa dakika 5 hadi 7.

20150118_132215

 • Kama hamira ikiumuka na kuwa kama utando juu ya maji (Kama maziwa yaliyochemka yanavyoweka cream juu), hapo ni vizuri unaweza kuendelea. Kama ikiwa imekatika, mwaga na rudia tena hatua ya kuweka sukari, hamira na maji. Cha msingi, hakikisha maji yana moto mzuri. (Nyuzi 40°C hadi 50°C). Usiendelee kuongeza vitu kama hamira haijachanganyika vizuri na maji.

20150118_133316

 • Weka unga kwa awamu. Chota kiasi na weka kwenye maji. Koroga hadi uchanganyike vizuri na maji.
 • Weka mafuta kisha koroga hadi yachanganyike vizuri.

20150118_133953

 • Pasua yai, weka kwenye bakuli. Koroga hadi lichanganyike vizuri.
 • Weka chumvi, maziwa ya unga,na vanilla. Koroga hadi mchanganyiko uwe na uwiano sawa.

Hii ndio hatua unayoweza kuongeza vikorombwezo unavyopenda viwe kwenye mkate wako. Kisha koroga.

 • Sasa anza kuongeza unga kidogo kidogo huku unakoroga hadi ichanganyike vizuri.
 • Kama unatumia wisk (Angalia hapa), koroga hadi ufikie hatua haiwezi tena kupita kati ya unga. Badilisha na utumie mwiko wa mbao. Hii itakuwa rahisi kuchanganya kama unasonga ugali.
 • Ongeza unga kidogo kidogo hadi pale ngano iliyolowa itakapoacha kunatia kwenye mwiko.

20150118_134826

 • Kwenye meza au ubao wako kwa kukandia, paka unga mkavu kiasi kisha weka ngano yako iliyochanganywa.
 • Kanda unga wako hadi ukamilike.
 • Weka mafuta ya kula kidogo kwenye bakuli kubwa (plastiki au kioo) kisha paka vizuri mafuta ndani ya bakuli.
 • Chukua unga uliomaliza kukanda, ingiza kwenye bakuli kisha geuza geuza ili upate kujipaka mafuta ya kula yaliyo kwenye kuta za bakuli.

20150118_141423

 • Acha unga kwenye bakuli. Funika na kitambaa chepesi juu kwa dakika 30 hadi 40 ili upate kuumuka.
 • Baada ya dakika 40, funua na kisha bonyeza unga ndani ili kutoa hewa iliyojaa. Binya vizuri hadi hewa yote itoke. Kisha funika tena kwa dakika nyingine 30 hadi 40.

20150118_151441

20150118_151612

3. Kuandaa mikate

 • Washa oven, weka nyuzijoto 180°C.
 • Unga ukishaumuka, toa kisha weka kwenye meza ya kukandia.

20150118_161505

 • Tandaza unga mkavu kiasi chini, kisha kanda tena ngano yako kidogo. Hii inasaidia kuondoa hewa iliyobaki ndani ya unga.
 • Gawa ngano kwenye mabonge machache kulingana na idadi ya mikate unayotaka.
 • Anza kutengeneza shepu unazotaka za mkate.

1

 • Changanya nyama ya kuku uliyoandaa. Weka kwenye mkate kisha funga vizuri.

2

3

5

6

 • Ukimaliza kufunga, pasua yai, koroga na changanya maji kidogo. Paka mchanganyiko wa yai juu ya mkate kisha mwagia ufuta.
 • Panga mikate kwenye chombo cha kuokea
 • Weka mikate kwenye oven. Acha iive kwa muda wa dakika 30 hadi 40.

7

 • Angalia mikate kama imeiva.
 • Jirambe

4

Unaweza kuhifadhi mkate huu vizuri kwenye jokofu kwa kufuata hatua zifuatazo:

 • Ila kabla ya kuweka kwenye jokofu hakikisha mkate umepoa kabisa
 • Funga mkate na mfuko wa nylon (Kuna mifuko laini ya nylon ya kuhifadhia chakula)
 • Weka kwenye jokofu
 • Wakati wa kutaka kuila, toa kwenye jokofu, acha ipoe kiasi, kisha nyunyizia maji na uweke kwenye microwave kwa dakika 1
 • Kisha weka mkate kwenye oven kwa dakika 5 hadi 7, na mkate utakuwa mzuri na mtamu kama umetoka kutengenezwa. 

MAPISHI YAPENDWAYO

Kuku wa mchuzi
dakika 25
Walaji: 4

Broccoli ya bamia
dakika 15
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.