Mkate wa ndizi na mayai

Mapishi haya rahisi ya mkate wa ndizi yanakupa kitafunwa kizuri kwako na familia. Unaweza kupika mkate huu kwa kutumia oven au hata jiko la mkaa. Yote yanawezekana, cha msingi ni kuelewa jinsi ya kuandaa tu.

Mahitaji

 • Unga wa ngano ¾ kilo
 • Mafuta ya kula ¼ lita
 • Sukari ½ kilo
 • Vijiko 2 vya chai vya hamira
 • Backing powder
 • Ndizi 3
 • Mayai 2
 • Chumvi ½ kijiko cha chai
 • Bakuli ya kuokea kwenye oven (au Sufuria ya kupikia kwenye jiko la mkaa)
 • Bakuli 4 – Ndogo (Kwa kupigia mayai), Wastani (Kupondea ndizi), Wastani (Kuchanganyia unga), Kubwa (Kuchanganyia kila kitu)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Leo tunaandaa mkate wa ndizi na mayai. Tukimaliza mapishi yetu mkate utaonekana kama:

20150113_210800

 • Washa oven kwenye nyuzijoto 350°F (180°C)
 • Changanya unga, sukari, backing powder na hamira pamoja. Changanya vizuri kwa pamoja.

20150111_152323

 • Pasua mayai kwenye bakuli, koroga vizuri. Hifadhi pembeni.

20150111_155633

 • Saga ndizi vizuri hadi ziwe uji. Hifadhi pembeni

20150111_160349

 • Kwenye bakuli kubwa, weka mafuta ya kula, kisha weka sukari kiasi na changanya kwa pamoja. Koroga hadi sukari iyeyuke.
 • Ongeza tena sukari hadi umalize sukari yote uliyotenga kwa ajili ya mkate.

20150111_155321

 • Mimina mayai kwenye bakuli yenye mchanganyiko wa mafuta na sukari. Koroga vizuri hadi mchanganyiko uwe sawia.

20150111_155719

20150111_155911

 • Weka mchanganyiko wa unga kiasi kwenye bakuli kubwa yenye mafuta na mayai. Koroga vizuri, hadi ichanganyike. Kisha ongeza ndizi zilizipondwa. Changanya zaidi. Fanya hivi hadi unga na ndizi zote zitumie. Hakikisha umechanganyika vizuri sana.

20150111_160606

 • Kwenye bakuli la kuoka – paka mafuta ili mkate usinate. (Mie hapa nilitumia aluminum foil paper)

oven-bakuli

bakuli-foil

 • Mimina mchanganyiko kwenye bakuli la kuokea. Kisha weka kwenye oven kwa dakika 75.

 

20150111_162318

20150111_162913

 • Baada ya dakika 75 toa mkate na weka kwenye sahani. Acha upoe na ukate kwa ajili ya kula.

Unaweza pia kupika mkate huu kwa kutumia jiko la mkaa kwa kupalilia makaa juu ya mfuniko ili mkate upate kupata moto vizuri juu na chini. Cha muhimu ni kuhakikisha moto unakuwa mwingi kwa kipindi chote ili upate matokeo mazuri zaidi.

20150111_174246

 • Jirambe na ladha ya maisha.

20150113_210800


MAPISHI YAPENDWAYO

Chips na nyama ya ng'ombe
dakika 25
Walaji: 2

Nyama tamu ya ng'ombe
dakika 40
Walaji: 4

Sambusa za mboga za majani
dakika 20
Walaji: 6

Toa maoni yakomadam K
18:04, Thu 15 Jan 2015

Je naweza tumia ngano isiyokobolewa na ukatoka vizuri tuu?

Dadia Msindai
18:39, Thu 15 Jan 2015

Asante kwa swali @Madam K,

Naweza kusema pia ni wazo zuri sana. Mie binafsi sijawahi kujaribu kutumia ngano isiyokobolewa, ila ningependa kufahamu matokeo yake pia.

Cha msingi kama ukitumia unga wa ngano unayopenda, matokeo yake yatakuwa mazuri tu. Mie binafsi naamini mapishi yanatakiwa yaendane na unachopendelea. Ukipenda kutumia ngano isiyokobolewa itakuwa vizuri pia, maana unapata virutubisho zaidi. Nadhani na mie  ntajaribu pia nikiandaa mara nyingine. Halafu ntakupa jibu. Kama utajaribu kabla yangu ntaomba unipe jibu, ili nami nifahamu.

Asante kwa swali lako, limenipa changamoto za kujaribu zaidi.

JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.