Mkate wa strawberry na chocolate

Mie hupenda kutumia muda wangu wa weekend kuandaa vitu vitamu, hasa ku-bake mikate, cake, maandazi na vingine. Niliwahi kuonja huu mkate kabla ya kuuandaa, na sikuweza kujizuia, ikabidi niandae tu ili nipate kuhisi tena ile ladha tamu. Hakika familia ilifurahia na tulijiramba hasa. Ni mkate ulio bora, rahisi kuandaa na hauhitaji ujuzi mkubwa sana, bali ni mapenzi yako na muda mchache sana. Jirambe

Mahitaji

 • Kikombe 1 cha strawberry (zilizokatwa vipande vidogo vidogo)
 • ¾ kikombe cha sukari (nimetumia sukari ya brown)
 • Kikombe 1 ½ cha unga wa ngano
 • ½ kikombe cha mafuta ya kula (Vizuri ukitumia mafuta asilia yanayotokana na mimea)
 • Mayai 2
 • ½ kikombe cha vipande vya chocolate
 • Kijiko 1½ cha mdalasini
 • ½ kijiko cha chumvi
 • ½ kijiko cha baking soda (Muhimusiyo hamira)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Leo tunaandaa mkate mtamu sana ulio na strawberry na chocolate. Tukimaliza, mkate utakuwa unaonekana na  utamu kama hivi:

chocolate_chip_strawberry_b

 • Kama unatumia oven, washa kwenye nyuzi joto 320°F (au 180°C) ili iweze kupata moto wakati unandaa mchanganyiko wa mkate
 • Changanya sukari, unga, mdalasini,  chumvi na baking soda kwenye bakuli kubwa na koroga vizuri

20150201_161237

 • Kwenye bakuli tofauti: weka mafuta ya kula, pasulia yai juu yake na koroga vizuri hadi vipate kuungana sawia

20150201_161204

20150201_161425

 • Ongeza vipande vya chocolate na strawberry kwenye bakuli yenye mchanganyiko wa mafuta na chocolate. Koroga vizuri ili vichanganyike.

20150201_154555

20150201_162025

 • Minipa rojo la mafuta na mayai kwenye unga. Koroga vizuri hadi lilainike vizuri.

20150201_162231

20150201_162737

 • Mimina mchanganyiko wako kwenye bakuli unalotumia kuoka kwenye oven.

20150201_163125

 • Weka bakuli kwenye oven, tega dakika 45 ili ipate kuiva.
 • Kama unatumia rice cooker, mimina mchanganyiko kwenye bakuli la rice cooker, kisha washa na tega saa 1 (kama linaruhusu) au likizima kabla ya muda endelea kuliwasha hadi muda wa saa 1 ufikie.
 • Baada ya dakika 45  (au saa 1 kama unatumia rice cooker) tumbukiza toothpick (kijiti kisafi cha kuchokonolea meno au njiti ya kiberiti) ili kuona kama mkate umeiva. Kikitoka kikavu, mkate umeiva, vinginevyo rudisha tena kwa dakika 5 hadi 10 ili upate kuiva.
 • Unaweza kula mkate huu ukiwa wa moto au baridi, utamu uko pale pale.

chocolate-bread-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.