Mlenda wa bamia na nyanya chungu

Mlenda ni mboga yetu cha asili. Kuna mlenda wa aina nyingi sana. Haya mapishi yanaonyesha mojawapo kati ya mlenda unayoweza kuandaa kutumia vitu rahisi – bamia na nyanya chungu, lakini ladha yake si ya kawaida. Inafaa zaidi kuliwa na ugali ukiwa wa moto na pilipili.

Mahitaji

 • Nyanya chungu
 • Bamia
 • Nyanya maji
 • Kitunguu
 • Karoti
 • Pilipili hoho
 • Mafuta ya kupikia

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Menya nyanya, kitunguu, karoti na pilipili hoho. Kata kwenye vipande vidogo.
 • Andaa bamia kwa kutoa ncha na mkia kisha kata mara mbili au jinsi utakavyopendezwa
 • Menya nyanya chungu na kuikata katikati.
 • Bandika sufuria kisha weka mafuta kiasi. Yakichemka weka nyanya chungu. Kaanga kama dakika kumi ili zibadilike rangi na kuwa za rangi ya udongo (angalia zisiungue). Kisha zitoe kwenye mafuta.
 • Punguza mafuta ya kula kiasi, bakiza yanayotosha kupikia mboga.
 • Weka kitunguu. Koroga na subiria kiive.
 • Weka pilipili hoho na carrot. Koroga kwa muda wa takribani dakika 3
 • Weka nyanya. Koroga na kisha funika ili ziive.
 • Weka bamia. Ongeza maji kiasi. Bamia huchukua muda kuiva, hivyo ni vizuri kuongeza maji.
 • Funika mboga yako na acha ichemke kwa muda wa dakika kama 10 – 15. Bamia zitakua zimeiva. Kuwa makini bamia zisilainike sana.
 • Weka nyanya chungu kwenye mchuzi. Acha zichemke kama dakika 5 kisha ipua mboga yako inakua tayari kuliwa.
 • Jirambe na ladha ya maisha, maisha ya kuteleza kama ulivyo mlenda

MAPISHI YAPENDWAYO

Kuku wa kuoka
saa 1
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.