Mlo mwepesi wa Salad ya sausage

Kula kwa afya ni muhimu, hasa pale unapokuwa unataka kula vizuri na kutotibua ratiba zako za kufanya kazi kwa ufasaha ukiwa ofisini. Salad ni chakula chepesi, kinakupa nguvu za kutosha na kuzuia adha zinazotokana na kushiba kupita kiasi. Salad hii ina nyama kiasi ambayo inaweza kukupa nguvu ziadi, hasa kwa wale wanaopenda kula nyama katika kila mlo. Jirambe na ladha ya maisha.

Mahitaji

 • Kabichi
 • Nyanya
 • Vitunguu
 • Spinach
 • Pilipili hoho
 • Olive oil
 • Limao au vinegar au ndimu
 • Chumvi kiasi
 • Sausages

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Anza kuandaa sausages. Chemsha na maji, weka chumvi kiasi na acha ziive.
 • Kata mboga za majani kwenye vipande vidogo. Weka kwenye sahani.
 • Kata nyanya, pilipili hoho, karoti kwenye vipande vidoho, kisha changanya na salad yako.
 • Kata sausages kwenye vipande vidogo na changanya kwenye salad
 • Changanya vinegar, limao au ndimu na olive oil pembeni kwenye bakuli. Unakoroga vizuri hadi ziwe sawia.
 • Nyunyuzia mchanganyiko wa limao au ndimu au vinegar na oil juu ya salad. Nyunyuzia kuzunguka salad, usirundike sehemu moja.
 • Weka chumvi kiasi kisha anza kuchanganya changanya
 • Kumbuka, salad inaliwa ikiwa ya baridi, so huna haja ya kupasha moto.

Bon appetit ;) na usisahau kushirikisha wale uwapendao kujiramba kwenye salad tamu, jirambe na ladha ya maisha.


MAPISHI YAPENDWAYO

Kamba wenye mboga za majani
dakika 15
Walaji: 2

Mapishi ya ndegu kwa watoto
dakika 60
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.