Mtori wa ndizi

Mtori ni chakula kizuri sana kwa mtoto, humsaidia mtoto kupata madini na virutubisho muhimu mwilini vinavyomsaidia kujenga mwili.

Mahitaji

 • Ndizi bukoba 2 kubwa zilizokomaa vizuri
 • Karoti 4
 • Butter vijiko 2
 • Kitunguu maji 1
 • Nyama robo
 • Supu ya nyama
 • Maziwa robo lita
 • Cream ya maziwa
 • Mdalasini robo kijiko cha chai
 • Nutmeg robo kijiko cha chai
 • Nyanya 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Bandika nyama jikoni, iive iwe laini na ibaki na supu.
 • Menya ndizi, nyanya, kitunguu na karoti.
 • Chukua sufuria, kata nyanya, ndizi,  karoti na kitunguu. Weka vyote kwenye sufuria moja.
 • Weka mdalasini, chumvi, butter na nutmeg kisha weka supu na nyama. Bandika jikoni.
 • Supu ikikaribia kuisha, weka cream, punguza moto acha ichemke kama dakika 5 kisha weka maziwa.
 • Epua, acha ipoe kisa saga. Ipashe kidogo mpe mtoto ale itakayobaki iweke kwenye jokofu.

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.