Ndizi bukoba zenye nyama, nazi na viungo

Mahitaji

 • Ndizi bukoba 15
 • nyama kilo 1
 • Nyanya 4
 • Vutunguu maji 2
 • Kitunguu saumu kijiko 1 cha chakula
 • Tangawizi kiasi
 • Giligilani ya unga kiasi
 • Curry powder kijiko 1 kikubwa cha chakula
 • Mafuta kiasi
 • Pilipili hoho 1
 • Karoti 1 kubwa
 • Tui la nazi kikombe 1 kikubwa
 • Supu ya nyama kias
 • Bizari kijiko 1 cha chai
 • Chumvi kiasi
 • Soy sauce kiasi
 • Nyanya ya kopo kijiko 1 cha chakula

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Kata nyama, osha kisha bandika jikoni. Nyama ikiiva epua weka pembeni.
 • Bandika sufuria, weka mafuta, kitunguu maji na viungo vyote. Kama saumu, hoho, bizari, giligilani, karoti, tangawizi na curry powder kaanga kwa dakika 3 kisha weka ndizi na nyama.
 • Pika ndizi na nyama kwa dakika 10, weka chumvi kisha weka nyanya ikiiza wka nyanya ya pakti na supu. Supu ikichemka weka soy sauce na tui la nazi acha tui lichemke.
 • Baada ya dakika 7, epua jirambe.

MAPISHI YAPENDWAYO

Sambusa za nyama
dakika 15
Walaji: 10

Macaroni ya cheese
dakika 20
Walaji: 3

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.