Ndizi bukoba zenye supu ya kuku na nyanya chungu

Hiki chakula ni kitamu na rahisi sana kumuandalia mtoto. Mtoto anapata virutubisho na madini mbalimbali vinavyosaidia katika ukuaji wake. Nyanya chungu zitamsaidia kumuongezea mtoto hamu ya kula.

Mahitaji

 • Ndizi bukoba nne
 • Supu ya kuku nusu lita
 • Nyanya chungu 6
 • Kitunguu saumu punje 5
 • Kitunguu maji 1
 • Nyanya maji 1 iliyoiza vizuri
 • Nutmeg nusu kijiko kidogo
 • Iliki nusu kijiko kidogo

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Andaa mahitaji - menya ndizi, nyanya chungu, nyanya maji, kitunguu na kitunguu saumu. Hakikisha supu ya kuku inakuwa tayari imeshaandaliwa.
 • Weka ndizi, nyanya chungu, nyanya maji, kitunguu maji na kitunguu saumu kwenye sufuria. Weka supu ya kuku kisha bandika jikoni.
 • Acha chakula kichemke kwa dakika 5 mpaka 7. Weka nutmeg na iliki. Supu ikianza kukauka na ndizi, nyanya chungu zikiwa zimelainika, epua, acha kipoe kiasi kisha mpe mtoto ajirambe.

misosi-kuku-ndizi-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Mapishi ya ndegu kwa watoto
dakika 60
Walaji: 1

Dagaa wa nazi na karanga
dakika 15
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.