Ndizi mshale za nazi

Mahitaji

 • Ndizi bukoba 20 zilizomenya vizuri
 • Nyama kilo 1 iliyopikwaa
 • Vitunguu maji 2
 • Giligilani kijiko 1 kikubwa
 • Gharam masala kijiko 1 cha chai
 • Nazi 1
 • Nyanya 4 zilizoiva
 • Kitunguu saumu 1
 • Nyanya ya pakti kijiko 1 kikubwa
 • Tangawizi kiasi
 • Chumvi kiasi
 • Karoti 1
 • Pilipili hoho 1
 • Curry powder kijiko 1 cha chakula

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Kwenye sufuria weka mafuta, bandika jikoni. Mafuta yakiwa tayari weka vitunguu maji pika kwa dakika 2 kisha weka kitunguu saumu, tangawizi, gharam masala, giligilani na curry powder, pika kwa dakika 1 kisha weka nyanya.
 • Pika nyanya iive mpaka nyanya itengane na mafuta, kisha weka nyanya ya kopo iache kwa dakika 1,weka ndizi, chumvi na nyama pika kwa dakika 10 kwa moto mdogo mpaka nyanya zigande kwenye ndizi.
 • Weka tui jepesi pika kwa dakika 7, kisha weka tui zito acha mpaka tui lipungue, katia pilipili hoho na karoti pika kwa dakika, epua, jirambe.

MAPISHI YAPENDWAYO

Brown rice, maziwa na karoti
dakika 60
Walaji: 1

Chicken Curry
dakika 30
Walaji: 3

Cornbread yenye korosho
dakika 40
Walaji: 6

Bata wa mchuzi wenye Bizari
dakika 40
Walaji: 6

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.