Ndizi mzuzu , kuku wa kuchoma na sauce ya nyanya

Mapishi haya yanakupa ladha ya kula ndizi mzuzu za kuchoma na kuchemsha wakati mmoja. Utaandaa tofauti lakini utakuja kula kwa pamoja ili kuona ladha yake.

Mahitaji

 • Nyanya 3
 • Kitunguu 1
 • Ndizi mzuzu zilivoiva 4
 • Mafuta ya kula
 • Kuku ½

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Andaa kuku – kata vipande unavyopendelea, muoshe, ongeza viungo unavyopendelea na kisha bandika jikoni. Acha achemke kwa muda mfupi kisha ipua na uhifadhi pembeni.
 • Menya ndizi 2 na zikate vipande vidogo.
 • Chukua ndizi 2 zilizobaki, kata ncha zake na kisha kata kwenye vipande viwili au vitatu vikubwa. Usimenye maganda ili iwe rahisi kuziivisha vizuri kwa kuchemsha.
 • Weka mafuta ya kula kwenye kikaangio au sufuria. Acha yapate moto vizuri.
 • Mafuta yakichemka, weka ndizi za kutosha. Angalia usirundike chakula, hakitoiva vizuri.
 • Bandika sufuria na maji jikoni na kisha weka vipande vya ndizi visivyomenywa.
 • Geuza ndizi za kwenye mafuta, zikiwa zimebadilika rangi na kuwa rangi ya udongo zitoe, na hifadhi kwenye chombo pembeni. Ongeza ndizi nyingine hadi umalize zilizobaki.
 • Andaa mchuzi wa nyanya na kitunguu kama unavyopenda. Unaweza kuongeza viungo unavyopenda, mfano unaweza kuweka pilipili hoho na bizari au royco kama unapendelea. Ili mradi upate mchuzi unaokufurahisha.
 • Usichanganye mchuzi na kitu kingine.
 • Kaanga kuku kwa kutumia mafuta ya ndizi. Acha ikaangike vizuri hadi ipate kuiva vizuri.
 • Chakula kikishaiva, pakua na weka kwenye sahani kwenye potions kidogo kidogo ili kula kwa staha.
 • Jirambe na ladha ya maisha.

MAPISHI YAPENDWAYO

Mtori wa ndizi
dakika 45
Walaji: 1

Pilipili ya maembe ya kusaga
dakika 35
Walaji: 5

Chicken with mashed potato
dakika 30
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.