Ndizi mzuzu na nyama ya kukaanga

Nyama ni chanzo kikubwa cha nyuzinyuzi pamoja na protini. Leo tunaandaa mapishi ya nyama ya kukaanga ikiwa na mchanganyiko wa viungo mbalimbali. Ili kukamilisha mlo wetu, tunaandaa nyama hii pamoja na ndizi mzuzu ambazo pia zimekaangwa kawaida kwenye mafuta. Karibu ujumuike nasi katika kuandaa chakula bora.

Mahitaji

 • Nyama ½ kilo - steki
 • Kitunguu saumu
 • Chumvi kijiko 1 cha chai
 • Limao au ndimu 1
 • Pilipili manga
 • Tangawizi 1
 • Vitunguu maji 2
 • Ndizi mzuzu 2
 • Olive oil
 • Basil

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Leo tunaandaa nyama ya kukaanga na ndizi mzuzu. Tukimaliza, chakula chetu kitaonekana kama hivi

20141215_204950

1. Andaa nyama

 • Kata nyama kwenye vipande vidogo wastani ila viwe vyembamba ili iwe rahisi kuiva. Kisha osha na weka kwenye bakuli la kuokea.

20141215_193509

20141215_194429

 • Nyunyiza limao na changanya vizuri.
 • Nyunyiza chumvi, kisha changanya vizuri
 • Weka kitunguu saumu, koroga vizuri ili ichanganyike vizuri
 • Weka tangawizi. Hii inasaidia kulainisha na vilevile kuleta ladha tamu
 • Weka pilipili manga (Fanya hivi kama unatumia pilipili)
 • Nyunyizia basil kuleta ladha na harufu tamu

20141215_200404

 • Hifadhi nyama kwa takribani dakika 30 hadi 45 ili viungo vipate kuingia vizuri.
 • Weka kikaangio jikoni, weka moto wa wastani na mafuta kiasi na acha ipate moto.
 • Weka vipande vya nyanya jikoni, acha viive kiasi na kisha geuza mara kwa mara. Hakikisha nyama inaiva vizuri kabla ya kuitoa, maana huchelewa sababu ni nyama inayopikwa bila kuchemsha.

20141215_201228

 • Mara kwa mara hakikisha nyama haiungui, geuze inapolazimu. Ikiiva tenga kwenye chombo pembeni. Rudia kwa vipande vyote vilivyobaki hadi utakapomaliza.

20141215_202457

 

2. Andaa ndizi wakati nyama inaiva

 • Menya na kisha kata ndizi mzuzu vipande vidogo

20141215_202230

 • Weka kikaangio jikoni, weka mafuta na subiria yapate moto
 • Weka ndizi jikoni, acha kwa muda ziive, kisha geuza ili zipate kuiva vizuri pande zote.

20141215_203239

 • Hakikisha usilundike ndizi kwenye kikaangia maana hazitoiva vizuri. Weka ndizi zinazotosha ili kupata matokeo mazuri;

20141215_203417

 • Ndizi zikiiva toa na weka kwenye chombo pembeni. Rudia kwa vipande vilivyobaki hadi umalize

3. Andaa chakula

 • Weka kwenye sahani, weka ndizi na kisha anza kujiramba

20141215_205019

20141215_205038

20141215_205011

Mlo mwema, karibu tena 


MAPISHI YAPENDWAYO

Tambi za sausage na kuku
dakika 45
Walaji: 2

Kuku wa kuoka na ndizi mzuzu
dakika 60
Walaji: 4

Salad yenye nyama ya kuoka
dakika 45
Walaji: 3

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.