Ndizi mzuzu na sauce ya ukwaju

Hii ni mojawapo ya njia za kuongeza ladha ya mapishi kwa kutumia juisi ya ukwaju. Ukwaju, kama ilivyo limao, hufanya ladha kuwa bora zaidi. Hizi ndizi zinaweza kuliwa na watu wa rika lolote – wakubwa kwa watoto. Ni chakula rahisi kuandaa na chepesi tumboni. Unaweza kula wakati wowote ule.

Mahitaji

 • Ndizi mzuzu 4
 • Bizari ¼ kijiko kidogo
 • Kitunguu saumu ½ kijiko kidogo
 • Mafuta kijiko 1 kikubwa 
 • Mbegu za mustard kijiko 1 kidogo
 • Bizari nyembamba kijiko 1 kidogo
 • Hing ¼ kijiko kidog
 • Iliki nusu kijiko cha chai
 • Curry powder ½ kijiko kidogo
 • Nazi au maji
 • Ukwaju vijiko 3 vikubwa
 • Chumvi kiasi au sukari au unaweza usiweke kabisa
 • Kitunguu maji 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Hii ni mojawapo ya njia za kuongeza ladha ya mapishi kwa kutumia juisi ya ukwaju. Ukwaju, kama ilivyo limao, hufanya ladha kuwa bora zaidi. Hizi ndizi zinaweza kuliwa na watu wa rika lolote – wakubwa kwa watoto. Ni chakula rahisi kuandaa na chepesi tumboni. Unaweza kula wakati wowote ule. 

 • Menya ndizi mzuzu, kata vipande vidogo vidogo. Bandika ndizi jikoni kwenye sufuria ya maji. Acha ziive hadi zilainike kabisa. Epua, acha zipoe kisha ponda. Hifadhi pembeni.
 • Kata kitunguu maji kwenye vipande vidogo.
 • Bandika sufuria jikoni. Weka mafuta ya kula. Mafuta yakipata moto weka mbegu za mustard, bizari nyembamba, hing, kitunguu maji, na curry powder. Koroga pamoja na pika kwa dakika 1.
 • Weka kitunguu saumu na iliki. Pika hadi kitunguu saumu kiive. Weka ndizi, chumvi (au sukari) kiasi na bizari. Pika kwa dakika 3.
 • Weka juisi ya ukwaju. Changanya vizuri. Kama anakula mtu mzima, unaweza kuweka cayyene pepper, mie nakula na mtoto hivyo sikutumia.
 • Epua, jirambe.

MAPISHI YAPENDWAYO

Ndizi mzuzu na sauce ya ukwaju
dakika 30
Walaji: 3

Samaki wa kupaka
dakika 60
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.