Ndizi mzuzu na sausage

Leo tunaandaa chakula chepesi na kitamu cha ndizi mzuzu na sausage. Hiki ni chakula chepesi na chenye ladha tamu. Ni maalumu kwa wale wanaume wanaobaki peke yao nyumbani na kuhisi uvivu wa kuandaa mlo mzuri, lakini afya na murua kwa kula wakati wa usiku maana hushibi hadi kuvimbiwa.

Mahitaji

 • Sausage 2
 • Cube maggie
 • Pilipili manga
 • Ndizi mzuzu 2
 • Olive oil

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Leo tunaandaa chakula kitamu kitakachoonekana kama hivi:

20141204_195453

 • Menya na kisha kata ndizi mzuzu vipande vidogo.

20141204_190937

 • Weka cube maggie kwenye ndizi mzuzu. Changanga vizuri ili iingie sawia.
 • Nyunyizia pilipili manga kwenye ndizi mzuzu.

20141204_191215

 • Weka kikaangio jikoni, weka mafuta na subiria yapate moto
 • Weka ndizi jikoni, acha kwa muda ziive, kisha geuza ili zipate kuiva vizuri pande zote.
 • Hakikisha usilundike ndizi kwenye kikaangia maana hazitoiva vizuri. Weka ndizi zinazotosha ili kupata matokeo mazuri;
 • Geuza ndizi mara tu zinapobadilika rangi na kuwa brown (rangi ya udongo)
 • Ndizi zikiiva toa na weka kwenye chujio lenye karatasi kama tissue ili kunyonya mafuta vizuri. Tissue wengine wanaita paper towel.

pic9

 • Rudia kwa vipande vilivyobaki hadi umalize

20141204_194933

 

 • Ukimaliza kuandaa ndizi, weka sausage kwenye kikaangio. Kisha geuza ili ziive vizuri. Halafu andaa chakula chako.

20141204_195504

20141204_195453


MAPISHI YAPENDWAYO

Grilled salmon
dakika 40
Walaji: 2

chilli chicken
dakika 30
Walaji: 3

Nyama ya kuoka na ndizi mzuzu
dakika 45
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.