Ndizi mzuzu zilizoiva

Mara nyingi tunakula ndizi mzuzu za kuchemsha, ukijaribu mapishi haya unaweza usile tena mapishi ya kawaida ya ndizi mzuzu. Utamu wake ni wa kipekee na hiki ni chakula bora, na hakina vikorombwezo vingi.

Mahitaji

 • Nazi 1
 • Ndizi mzuzu zilivoiva 6
 • Sukari kijiko 1 cha chai
 • Hiliki

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Menya ndizi na zikate kwa urefu ili utoe ule uzi mweusi katika kiini cha ndizi. Usitupe maganda.
 • Menya hiliki na kisha zitwange
 • Kuna nazi na uchuje tui zito na jepesi.
 • Katika sufuria ya kupikia, panga maganda ya ndizi mzuzu,vizuri na kisha juu yake panga ndizi kwa ufasaha.
 • Bandika sufuria jikoni na kisha weka tui jepesi. Acha kwenye moto ichemke hadi tui likauke.
 • Nyunyuzia sukari kidogo kwenye ndizi na weka hiliki.
 • Weka tui zito kisha ache lichemke kwa moto mdogo sana hadi tui likauke.
 • Unaweza kuepua na kujiramba.

MAPISHI YAPENDWAYO

Dagaa wa kuunga na nazi
dakika 18
Walaji: 2

Roast ya maini
dakika 30
Walaji: 2

Toa maoni yakowitness shayo
09:42, Fri 03 Jul 2015

Napenda mapishi yako naomba uwe unantumia through my email .

JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.