Ndizi utumbo za nazi

Ndizi ni chakula kitamu sana na ni rahisi kupika. Ndizi ni chanzo kizuri sana cha vitamin C, vitaminB6 na potasium. Virutubisho hivi ni muhimu sana katika mwili wa binadamu.

Mahitaji

 • Ndizi
 • Utumbo kilogram 1
 • Nazi kubwa iliyokomaa vizuri
 • Kitunguu maji
 • Tangawizi
 • Kitunguu saumu
 • Limao au Ndimu
 • Chumvi
 • Carry powder kijiko 1 cha chakula
 • Mdalasini nusu kijiko cha chai
 • Coriander powder nusu kijiko cha chai
 • Pilipili manga iliyosangwa
 • Nyanya

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Safisha utumbo vizuri sana hakikisha umetoa uchafu wote, weka kwenye sufuria au pressure cooker kama unalo weka chumvi, limao, tangawizi, kitunguu saumu na maji kiasi .
 • Bandika utumbo kwenye jiko.
 • Hakikisha hayo maji yataivisha utumbo na supu itabaki basi ukiiva epua weka pembeni.
 • Menya ndizi zikate kate vipande vidogo weka katika sufuria katia vitunguu maji, nyanya kisha mwagia supu uliyochemshia utumbo.
 • Bandika jikoni funika zikikaribia kuiva weka utumbo kisha weka viungo vyote amabavyo hujaviweka viweke kwenye ndizi.
 • Mwagia tui la nazi zito subiri lichemke kama dakika kumi na tano , changanya sasa hapo chakula kitakua tayari kwa kujiramba.

MAPISHI YAPENDWAYO

Dagaa wa kuunga na nazi
dakika 18
Walaji: 2

Roast ya maini
dakika 30
Walaji: 2

Kebab za nyama
dakika 15
Walaji: 3

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.