Ndizi za kuoka kwa kupakwa asali

Chakula hiki ni kitamu, rahisi kuandaa na kinavutia. Hisia zake unaweza kufumba macho kila unapomega kipande cha ndizi na kuingizia mdomoni. Ni raha iliyozidi kifani. Jaribu kuandaa na uone raha yake, hakika utafurahia.

Mahitaji

  • Ndizi 2 (Mie nimetumia ndizi mzuzu, ila unaweza pia kutumia ndizi za kuiva kawaida)
  • Asali vijiko 4
  • Karanga zilizokaangwa ¼ kikombe
  • Mtindi (Vizuri kama utakuwa na mtindi usio na sukari. Mtindi utasaidia kuzuia kasi ya unyonywaji wa sukari kwenda kwenye damu)
  • Kijiko 1 cha chai cha mdalasini

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Huu ni mlo mtamu na rahisi kuandaa na pia hauna kalori nyingi sana kama hupendi kushiba mno. Lakini kuwa makini, ndizi na asali zina sukari nyingi sana, hivyo si vizuri kuliwa na mtu ambaye ana matatizo ya sukari. Uwepo wa karanga na mdalasini husaidia kupunguza unyonywaji wa sukari kwenye damu lakini isiwe kigezo cha kula sana, maana miili inatofautiana.

misosi-ndizi-asali-main

  • Washa oven kwenye nyuzijoto 190°C (370°F) acha ipate moto vizuri wakati unandaa ndizi.
  • Andaa sinia au bakuli ya kuokea kwenye oven. Weka foil paper juu yake, maana asali inanata sana. Ni bora inate kwenye foil paper kuliko bati.
  • Menya ndizi kisha kata katikati kwa urefu. Panga juu ya chombo cha kuokea. Mwagia asali, paka vizuri pande zote mbili. Mwagia mdalasini kisha paka vizuri pande zote mbili. Weka chombo cha kuokea kwenye oven. Tega muda wa dakika 10 hadi 15. Angalia zisiungue.
  • Baada ya ndizi kuiva vizuri, toa na kisha panga kwenye sahani. Mwagia karanga juu yake. Unaweza kula ndizi hizi na mtindi.
  • Jirambe

misosi-ndizi-asali-other


MAPISHI YAPENDWAYO

Cornbread wenye zabibu kavu
dakika 40
Walaji: 3

Paella
dakika 30
Walaji: 8

Beef Rendang
dakika 60
Walaji: 5

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.