Ndizi za kuunga na nazi

Kuna aina tofauti za ndizi – malindi, mkono wa tembo, bukoba, na nyingine kibao. Haya mapishi unaweza kupika aina yeyote ya hizo ndizi, ili mradi tu ziwe hazijaiva. Uwepo wa nazi kwenye hiki chakula unahakikisha uhalisia wa ladha na utamu wa kipekee. Unaweza kula hizi ndizi kama kitafunwa cha chai, chakula kamili au chakula kiambato ukiwa na chakula kingine mfano wali, tambi au ugali.

Mahitaji

 • Ndizi mbichi 6
 • Nazi 1
 • Vitunguu 2
 • Pilipili hoho 1
 • Karoti 2
 • Nyanya 3
 • Chumvi kijiko 1 kikubwa

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Menya ndizi kisha ziweke kwenye maji. Hii inasaidia kutopata weusi na utomvu unaotokana na kutokuwa kwenye maji. Kisha osha ndizi zako na uweke tena kwenye chombo chenye maji mengi.
 • Menya vitunguu na kisha katakata vipande vidogo.
 • Kata pilipili hoho, menya nyanya uzikate vipande.
 • Kata karoti na nyingine kwangua maganda.
 • Andaa nazi kwa kuikuna na kukamua tui 2 – moja tui zito weka kwenye chombo pembeni na tui jepesi kwenye chombo tofauti.
 • Bandika chungu au sufuria ya kupikia jikoni. Ongeza tui zito kidogo, acha lichemke mpaka litoe mafuta.
 • Tui likishatoa mafuta, weka vitunguu vyako mpaka vikaribie kuiva halafu ongeza pilipili hoho. Koroga kiasi halafu weka karoti. Endelea kukoroga mchanganyiko kwa dakika 2 halafu ongeza nyanya kwenye sufuria. Ongeza chumvi na kisha funika sufuria na mfuniko hadi nyanya ziive (takribani dakika 5 hadi 8).
 • Nyanya zikiiva, ongeza ndizi kwenye sufuria yenye viungo. Endelea kukoroga.
 • Ongeza tui jepesi kwenye sufuria yenye ndizi huku unaendelea koroga ili tui lisikatike.
 • Ikishachemka, ongeza na kupungua tui, ongeza tui zito huku ukiendelea koroga mpaka lichemke.
 • Acha mchanganyiko uchemke kwa takribani dakika 10 ili tui liive.
 • Ndizi zako zitakua zimeiva.

Jirambee na ladha ya maisha..! Enjoy ndizi za kupika.


MAPISHI YAPENDWAYO

Sausage Stroganoff
dakika 10
Walaji: 2

Mkate wa boga
dakika 60
Walaji: 5

Njegere za nazi na maziwa
dakika 35
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.