Ndizi za utumbo nazi na karanga

Pishi hili ni tamu na ni rahisi kuandaa, utapata vionjo vya nazi na karanga kwa pamoja.

Mahitaji

 • Ndizi bukoba 8, menya kisha kata vipande unavyopenda. Kama una chombo     kikubwa unaweza kuacha ndizi nzima.
 • Utumbo nusu (½) kilo
 • Karanga robo (¼) kilo
 • Pilipili mbuzi 1
 • Nyanya 4, menya na kata vipande vidogo au saga.
 • Mafuta vijiko 2 vya chakula
 • Chumvi
 • Nazi 1, pasua, kisha kuna na tengeneza tui
 • Kitunguu maji 1, menya na kata vipande vidogo

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Mapishi haya ni yameandikwa na @officialmwana. Tunashukuru kwa mchango wako wa dhati ili kuendelea kuchangia elimu juu ya mapishi.

 • Safisha utumbo vizuri, osha kisha weka kwenye sufuria au chombo utakachotumia kupikia. Weka chumvi, bandika jikoni, acha uive vizuri ila ubaki na supu kiasi.
 • Kwenye sufuria tofauti, weka mafuta. Bandika jikoni. Mafuta yakipata moto, weka utumbo, bila mchuzi, kisha kanga vizuri. Weka ndizi na kitunguu maji, endelea kukaanga kwa dakika nyingine 5. Weka supu au mchuzi wa utumbo kwenye sufuria. Koroga pamoja. Funika acha ichemke.
 • Mchuzi ukikaribua kukauka, weka nyanya. Koroga vizuri kisha funika acha dakika 3 ziive.
 • Weka karanga, tui la nazi, pilipili hoho na karoti. Tupia na pilipili kuongeza ladha na harufu tamu. Koroga taratibu ili tui lisikatike, usiache hadi lianze kuchemka.
 • Tui la nazi likichemka vizuri acha kwa dakika 3 hadi 5 kisha epua ujiraaambe kwa raha zako.

MAPISHI YAPENDWAYO

Kuku wa broccoli
saa 1
Walaji: 4

Mchuzi wa biryani
dakika 35
Walaji: 3

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.