Nyama tamu ya kukaanga

Mapishi haya ya nyama ya kukaanga ikiwa na viungo yanakupa matokeo mazuri ya nyama laini, tamu na yenye harufu nzuri. Kama unavyoiona inavyovutia, ndio itakavyokuwa ukiwa unaing'ata taratibu huku ikiwa inakupa utamu na ladha maridadi kabisa. Ni vizuri ukipika na kuona matokeo yake.

Mahitaji

 • Nyama kilo 1
 • Ndimu 1
 • Chumvi nusu kijiko kidogo
 • Kitunguu saumu 1
 • Kitunguu maji 1
 • Tangawizi kijiko 1 cha chakula
 • Soy sauce kijiko 1 kidogo
 • Mafuta ya kula

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Hadi muda naandika jinsi ya kuandaa hii nyama nilikuwa naitamani tena kuila. 

 • Kata nyama, osha vizuri, weka chumvi na ndimu kisha bandika jikoni. Hakikisha nyama imeiva vizuri na mchuzi umeishia. Epua.
 • Weka kitunguu swaumu na tangawizi kwenye nyama. Kwangua kitunguu maji weka kwenye nyama. Weka soy sauce kiasi. Acha nyama kwa muda wa dk tano.
 • Bandika frying pan jikoni, weka mafuta ya kula. Mafuta yakipata moto weka nyama. Punguza moto uwe wa wastani. Pika nyama kwa moto mdogo maana hii nyama haitakiwi kukauka sana.
 • Geuza kila mara kama dakika 10, epua. Jirambe.

misosi-nyama


MAPISHI YAPENDWAYO

Ndizi mzuzu na sauce ya ukwaju
dakika 30
Walaji: 3

Samaki wa kupaka
dakika 60
Walaji: 2

Cheese Burger
dakika 15
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.