Nyama tamu ya ng'ombe

Inawezekana umeshapika nyama kwa mapishi tofauti, lakini pishi hili pia litakupa matokeo mazuri. Ni mboga nzuri unayoweza kupika kwa kulia na ugali, wali, maandazi, mihogo, au vyakula vingine tofauti. Uwepo wa viungo huipa mboga hii ladha tamu na harufu nzuri ya kukuvutia kula kwa furaha.

Mahitaji

 • Nyama ½ kilo
 • Kitunguu saumu 1, menya kisha saga
 • Pilipili hoho 1, kata vipande vidogo
 • Karoti 1, menya kisha kata vipande
 • Chumvi ½ kijiko cha chai
 • Bizari nyembamba kijiko 1 cha chai
 • Soy sauce vijiko 3 vya chakula
 • Apple cider vinegar
 • Tomato sauce nusu kikombe
 • Nyanya 2, menya kisha kata vipande vidogo, au saga
 • Kitunguu maji, menya kisha kata vipande vidogo

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kuwa huru kuongeza au kupunguza viungo unavyopenda kwenye mboga hii.

 • Andaa nyama – osha kisha kata vipande vizuri. Nyunyizia vinegar, sauce na chumvi. Bandika jikoni kisha acha ichemke mpaka iive. Epua na hifadhi pembeni.
 • Bandika sufuria jikoni, weka mafuta ya kula. Mafuta yakipata moto weka kitunguu maji, kitunguu saumu na bizari nyembamba. Koroga pamoja, acha vichemke. Baada ya dakika 2 weka nyanya, koroga pamoja. Acha nyanya ziive hadi zianze kutengana na mafuta. 
 • Weka nyama, bila supu, pika mpaka nyanya zigandie vizuri kwenye nyama. Weka pilipili hoho na karoti. Weka supu ya nyama kiasi kisha acha nyama ichemke hadi mchuzi ubaki kidogo. Weka tomato sauce, koroga vizuri. Acha ichemke kwa pamoja kwa dakika 5 zaidi.
 • Epua mboga na itakuwa tayari kuliwa.
 • Hii mboga inafaa kuliwa na chapati, maandazi, ugali, wali na vingine.  Ili kupata ladha zaidi, tumia pia mboga majani wakati unakula nyama ili kupata mlo kamili.

nyama-mchuzi


MAPISHI YAPENDWAYO

Chocolate pancakes
dakika 15
Walaji: 6

Vitumbua vya mayai
dakika 10
Walaji: 6

Brown rice, maziwa na karoti
dakika 60
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.