Nyama tamu yenye pilipili

Hii nyama tamu yenye pilipili (au beef chilli ), ni mboga rahisi ya kuwapa chakula kitamu, kizuri na kilicho na ladha maridhawa wale wote uwapendao. Ni haraka kuandaa na matokeo ni mazuri sana. Jaribu leo upate kuona utamu wake.

Mahitaji

 • Nyama ½ kilo
 • Soy sauce vijiko 3 vya chakula
 • Chili sauce kijiko 1 cha chakula
 • Nyanya ya kopo 1 kijiko kimoja
 • Pilipili manga vijiko 2 vya chakula
 • Tangawizi 1
 • Kitunguu saumu 1
 • Pilipili mbuzi 3
 • Vitunguu maji 2
 • Chumvi kijiko 1 kidogo
 • Royco
 • Mafuta ya kula
 • Majani ya thyme na parsley
 • Unga wa mahindi ½ kijiko cha chai

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Unaweza kuandaa nyama hii na kuhifadhi ili kula wakati tofauti. Mara nyingi mboga zikikaa huwa zinaongeza ladha.

 • Andaa nyama – kata na osha vizuri. Bandika nyama jikoni, weka chumvi. Pika hadi iive vizuri. Ikishaiva itoe na hifadhi pembeni.
 • Wakati nyama inaiva andaa kitunguu saumu, kitunguu maji na pilipili mbuzi. Menya na kata vizuri kisha hifadhi vizuri pembeni.
 • Bandika sufuria tofauti jikoni. Weka mafuta, tangawizi, kitunguu saumu, vitunguu maji na pilipili mbuzi. Koroga vizuri, acha ziive kwa dakika 3 hadi 5. Hakikisha moto ni mkali ili mboga za majani zisichuje maji.
 • Weka nyama kwenye sufuria yenye mboga za majani. Koroga vizuri.
 • Weka majani ya thyme, koroga. Weka soy sauce, chill sauce na nyanya ya kopo kisha koroga taratibu ili mchanganyiko uwe sawia. Unaweza kufanya hivi kwa dakika 7 ili nyama isigande.
 • Weka unga wa mahindi, koroga kwa dakika 2. Weka pilipili manga, royco, na majani ya parsely. Koroga vizuri na funika. Acha ichemke vizuri kwa takribani dakika 3 hadi 5 kisha endelea kukoroga.
 • Nyama itakuwa tayari imeiva na unaweza kujiramba.
 • Unaweza kula nyama hii na vyakula tofauti – ugali, wali, ndizi, au kingine unachopendelea. Unaweza pia kula kama kitafunwa kwa kuchangamsha mdomo.

misosi-beef-chilli-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Samaki wa kupaka
dakika 25
Walaji: 2

Tambi za hiliki na sukari
dakika 8
Walaji: 2

Ndizi za kuunga na nazi
dakika 20
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.