Nyama tamu yenye viungo tofauti

Nyama ya mapishi tofauti yenye viungo mbalimbali kuongeza utamu na kukupa ladha zaidi. Haya ni mapishi mazuri kwa kula na vyakula mbalimbali.

Mahitaji

 • Nyama steki kilo 1

Viungo vya kulainishia nyama

 • Paprika kijiko 1 cha chai
 • Bizari nyembamba ½ kijiko cha chai
 • Nutmeg ½ kijiko cha chai
 • Giligilani ½ kijiko cha chai
 • Mafuta vijiko 2 vya chakula
 • Garam masala ½ kijiko cha chai
 • Iliki ½ kijiko cha chai
 • Pilipili ndefu 1
 • Limao ½
 • Kitunguu saumu 1, kimenywe na kupondwa

Mahitaji ya kupikia nyama

 • Tangawizi kiasi
 • Curry powder kiasi
 • Bizari kiasi
 • Giligilani nusu kijiko  cha chai
 • Vitunguu saumu 2
 • Karoti 1
 • Pilipili hoho 1
 • Nyanya maji 4, ziwe zimeiva vizuri
 • Garam masala ½ kijiko cha chai
 • Chumvi ½ kijiko cha chai

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Ili kuifanya hii nyama iwe tamu zaidi, hakikisha unaiacha ikae kwenye viungo kwa muda mrefu zaidi ili iwe laini na kuongeza utamu. Unaweza kuongeza au kupunguza viungo kulingana na upendavyo.

 • Andaa nyama kwa kuikata vipande vyembamba na virefu, osha kisha weka pembeni ichuje maji. Weka viungo vya kulainishia nyama kwenye bakuli, changanya vizuri kisha weka nyama. Changanya nyama na viungo hadi nyama yote ienee viungo vizuri. Hifadhi nyama yenye viungo kwenye mfuko wa plastiki kisha weka kwenye jokofu (fridge) usiku mzima ili nyama ilainike vizuri na rahisi kuiva.
 • Ukiwa tayari kupika – bandika sufuria jikoni, weka mafuta ya kula, acha yapate moto vizuri kisha weka vitunguu maji. Koroga. Vikianza kubadilika rangi weka tangawizi, curry powder, bizari, giligilani, kitunguu saumu na garam masala pika kwa dakika 2 kisha weka nyama. Kaanga nyama na viungo kwa dakika 20.
 • Weka nyanya pika mpaka iive, ongeza maji kiasi na chumvi. Funika acha nyama ichemke kwa dakika 10. Weka karoti na pilipilipi hoho, koroga na kisha funika acha iive kwa muda wa dakika 5.
 • Epua mboga, itakuwa tayari kuliwa.
 • Unaweza kula mboga hii na vyakula aina tofauti – ugali, wali, maandazi, mihogo au chakula chochote unachopendelea. Jirambe na ladha tamu ya nyama.

misosi-nyama-two


Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.