Nyama ya kuchoma ya kusisimua ulimi

Nyama choma ni nzuri ukiwa unakunywa na vinywaji vikali au bia. Lakini si lazim, unaweza pia kula pamoja na chakula kikuu au kutumia kama kichangamsha kinywa unapokuwa unasogoa na rafiki au familia. Mie huwa napenda kula hii nyama kwa kachumbari ya nyanya pamoja na tango huku nikisindikizwa na chachandu na pilipili kali.

Mahitaji

 • Nyama ya ngombe kilo 1 (au kuku mzima)
 • Tangawizi 1 
 • Kitunguu swaumu 1
 • Karoti 2
 • Ndimu 1
 • Pilipili manga ya kusaga
 • Chumvi

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Menya tangawizi,vitunguu maji,vitunguu swaumu na karoti.
 • Weka kila akitu kwenye blender. Saga kwa pamoja ili kupata uji mzito.
 • Weka pilipili manga kwenye mchanganyiko wako.
 • Chukua nyama (Kuku, ng’ombe au nyingine unayopenda) kisha weka chumvi.
 • Kamulia ndimu au limao la kutosha kwenye nyama na kisha changanya kiasi.
 • Weka nyama kwenye mchanganyiko wako uliotoka kwenye blender.
 • Weka nyama kwenye jokofu kwa muda wa  saa moja au mawili. Unaweza pika kuandaa usiku na kuiacha kwenye jokofu ilale hadi asubuhi.
 • Andaa mkaa wako kwenye jiko la kuchomea.
 • Moto ukikolea vizuri, weka nyavu ya kuchomea na tandaza nyama yako kwenye nyavu.
 • Igeuze mara kwa mara ili iive vizuri pande zote.  
 • Ikishaiva vizuri, weka kwenye foil paper ili kuzuia kukauka.
 • Ukishamaliza kuchoma unaweza kula. Usisahau pilipili, ndimu au limao wakati wa kula.

MAPISHI YAPENDWAYO

Carrot cake
dakika 60
Walaji: 4

Grilled salmon
dakika 40
Walaji: 2

chilli chicken
dakika 30
Walaji: 3

Toa maoni yakogood beatus
12:23, Fri 15 Apr 2016

Nimependa material yako.

Naomba ushauri, nataka kufungua sehemu ya kuuza nyama Choma. Naomba unishauri niuze vitu ganii?

JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.