Nyama ya kuoka na ndizi mzuzu

Kuna aina nyingi za mapishi ya nyama. Hapa leo tunaangalia nyama ya kuoka kwa kutumia viungo mbalimbali. Kisha tunakula nyama hii na ndizi mzuzu ambazo zimekaangwa kawaida kwenye mafuta. Karibu ujumuike nasi katika kuandaa chakula bora.

Mahitaji

 • Nyama ½ kilo - steki
 • Kitunguu saumu
 • Chumvi kijiko 1 cha chai
 • Limao au ndimu 1
 • Pilipili manga
 • Tangawizi 1
 • Vitunguu maji 2
 • Ndizi mzuzu 2
 • Olive oil
 • Mustard (hadalari)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Tunaandaa mapishi haya kwa hatua 2 muhimu kabla ya kuchanganya na kuanza kula chakula hiki.

1. Andaa nyama

 • Kata nyama kwenye vipande vidogo wastani. Kisha osha na weka kwenye bakuli la kuokea.

20141215_193509

20141215_194410

 • Nyunyiza limao na changanya vizuri.
 • Nyunyiza chumvi, kisha changanya vizuri
 • Weka kitunguu saumu, koroga vizuri ili ichanganyike vizuri
 • Weka tangawizi. Hii inasaidia kulainisha na vilevile kuleta ladha tamu
 • Weka pilipili manga (Fanya hivi kama unatumia pilipili)

20141215_195948

 • Weka mustard, paka vizuri nyama zote
 • Kata vitunguu maji, weka vizuri kwenye bakuli na changanya kiasi na viungo

20141215_201302

 • Hifadhi nyama kwa takribani dakika 30 hadi 45 ili viungo vipate kuingia vizuri.
 • Baada ya dakika 45, washa oven kwenye nyuzi 250°C na acha lipate moto kwa takribani dakika 10.
 • Weka bakuli lenye nyama kwenye oven na tega muda dakika 45.
 • Mara kwa mara hakikisha nyama haiungui, geuze inapolazimu.

20141215_205316

2. Andaa ndizi wakati nyama inaiva

 • Menya na kisha kata ndizi mzuzu vipande vidogo
 • Weka kikaangio jikoni, weka mafuta na subiria yapate moto
 • Weka ndizi jikoni, acha kwa muda ziive, kisha geuza ili zipate kuiva vizuri pande zote.
 • Hakikisha usilundike ndizi kwenye kikaangia maana hazitoiva vizuri. Weka ndizi zinazotosha ili kupata matokeo mazuri
 • Ndizi zikiiva toa na weka kwenye chombo pembeni. Rudia kwa vipande vilivyobaki hadi umalize

3. Tenga chakula

 • Baada ya muda toa nyama yako iko tayari kuliwa
 • Weka kwenye sahani, weka ndizi na kisha anza kujiramba

20141215_210459

20141215_210603

20141215_210721


MAPISHI YAPENDWAYO

Ndizi mzuzu na sauce ya ukwaju
dakika 30
Walaji: 3

Samaki wa kupaka
dakika 60
Walaji: 2

Cheese Burger
dakika 15
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.