Nyama ya kusaga, sausage na mayai

Hiki ni chakula chepesi, kilichojaa protini ya kutosha. Ni mlo safi kula wakati wowote ule, iwe na chai, mchana au usiku. Ni mlo mzuri zaidi kwa usiku sababu ni chakula kisicho kizito na kinakufanya ujisikie faraja baada ya kula kwa kuweza kulala vizuri bila kuvimbiwa.

Mahitaji

 • Mayai 2
 • Sausage 2
 • Nyama ya kusaga gramu 200
 • Kitunguu saumu kijiko 1 kidogo
 • Tangawizi ya unga ½ kijiko kidogo
 • Pilipili manga ½  kijiko kidogo
 • Kitunguu maji 1
 • Chumvi
 • Pilipili hoho 1(Unaweza kutumia ½ zikiwa mbili za rangi tofauti )
 • Mafuta  ya kula

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Je una muda mchache wa kuandaa chakula na unapenda kula chakula rahisi kilichojaa virutubisho murua kwa afya yako ? Hiki ni mojawapo ya vyakula vichache unavyoweza kula.

 • Pasua mayai, koroga vizuri. Weka pilipili manga, chumvi na kitunguu saumu kidogo sana. Koroga vizuri hadi vichanganyike pamoja. Hifadhi pembeni.
 • Kata pilipili hoho kwenye vipande vidogo. Menya kisha kata kitunguu maji kwenye kipande vidogo.
 • Weka kikaango jikoni. Acha kipate moto vizuri, weka mafuta ya kula kidogo. Weka kitunguu saumu na kitunguu maji. Weka nyama ya kusaga, kaanga kwa kuikoroga mara kwa mara, usiiache maana itaungua kirahisi. Nyama ikishaanza kuiva na kubadilika rangi, weka pilipili hoho k iasi. Acha nyingine kwa ajili ya mayai. Koroga vizuri kisha acha ziive kwa dakika chache. Mie huwa napenda pilipili hoho zisiive sana, hivyo naziweka kwenye moto kwa dakika 3 hadi 5 na kuepua kikaango.
 •  Bandika kikaango jikoni, acha kipate moto vizuri. Weka mafuta ya kula kidogo sana. Weka kitunguu maji, koroga vizuri. Weka pilipili hoho zilizobaki kisha koroga. Weka mayai na acha yaive vizuri upande mmoja. Unaweza kuvuruga kama unapenda mayai yaliyochembuka. Au acha yaive vizuri kama unapenda mayai yaliyoshikana vizuri. Geuza upande wa pili kisha epua na uweke pembeni.
 • Unaweza kuandaa sausage kwa kukaanga kama huna shida na mafuta au unaweza kukaanga ili kuepuka mafuta. Mie nilichemsha tu ili kupata chakula mchanganyiko.
 • Tenga chakula chako na jirambe vizuri.

misosi-mayai-nyama-sausage-


MAPISHI YAPENDWAYO

Tambi na mayai
dakika 10
Walaji: 1

Samaki wa ngano na tangawizi
dakika 15
Walaji: 2

Kuku wa limao
dakika 45
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.