Nyama ya mbuzi kwa mapishi tofauti

Tunakula ili kujenga mwili, si kushiba peke yake. Je unafahamu mapishi yanayokufanya kujenga misuli mwilini ? Basi ndio haya. Nyama hii inayopikwa ili kuwezesha kuhifadhi virutubisho vyote na kuwa tayari kutumika mwilini mwako. Jaribu mapishi haya na familia, si kuongeza ladha tu bali kuleta mabadiliko katika mapishi.

Mahitaji

 • Nyama ya mbuzi – kilo 1
 • Vitunguu maji vikubwa - 2.
 • Nyanya za kawaida - 6 (ukipenda unaweza nunua na ya kopo).
 • Kitunguu swaumu - 1
 • Tangawizi
 • Karoti
 • Hoho
 • Kolimaua
 • Njegere
 • Mafuta
 • Chumvi
 • Maji
 • Bizari
 • Viazi ulaya

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Katakata nyama, osha kisha weka vitunguu swaumu na tangawizi. Ache nyama pembeni kama nusu saa ili viungo viingie vizuri.
 • Andaa karoti, vitunguu, nyanya, kwa kukata vipande vidogo vidogo.
 • Menya viazi, osha, kata vipande vidogo kisha hifadhi kwenye sufuria ya maji ili visibadilike rangi.
 • Andaa tangaziwi, vitunguu swaumu kwa kukata na kisha kuponda kwenye kinu
 • Bandika mafuta yakichemka tia vitunguu maji vyote vikaange mpaka viwe vinakaribia kubadilika rangi
 • Weka nyama ya mbuzi huku unaendelea kukoroga
 • Weka chumvi, koroga ili ichanganyike vizuri.
 • Weka pilipili hoho, carrots, kolimaua na njegere. Koroga kwa takribani dakika tano.
 • Weka nyanya koroga kiasi na kisha funika na mfuniko.
 • Mchanganyiko ukiiva weka nyanya ya kopo na maji kiasi ili kuivisha nyama.
 • Weka viazi ili vipate kuiva na mchanganyiko wa nyama.
 • Ili kuongeza ladha, weka bizari (au kiungo chochote cha kuongeza ladha ya chakula).
 • Funika nyama yako kwa muda wa dakika ishirini.

Nyama itakuwa tayari imeiva na unaweza kula na chakula upendacho.

Jirambe na ladha ya maisha, usisahau kushare na wenzio mapishi mazuri


MAPISHI YAPENDWAYO

Mboga ya majani mchanganyiko
dakika 10
Walaji: 4

Omelette za pilipili hoho
dakika 5
Walaji: 1

Kuku wa mboga za majani
dakika 15
Walaji: 2

Ndizi mzuzu na sausage
dakika 10
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.