Nyama ya ng'ombe ya kukaanga yenye utamu wa kipekee

Ukipenda kula nyama, hapa utafurahia. Uzuri wa mapishi haya hayahitaji uzuri mwingi wala muda mrefu. Maelezo machache, matokeo yake yatakushangaza. Ukiwa umetulia nyumbani, bila ya haja ya kuwa na jiko kubwa, jaribu kupika hii nyama. Utapata kujua utamu wake halisi.

Mahitaji

 • Nyama  - kilo 1
 • Mafuta ya kula - 1/2 lita
 • Chumvi 
 • Ndimu (Limao au vinegar) 1
 • Tangawizi  - 1
 • Kitunguu saumu  - 1
 • Cube magic
 • Viazi - 6
 • Viungo vingine upendavyo kwenye sauce*.

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Tayarisha nyama yako - kata, osha.
 • Weka limao, ndimu au vinegar kwenye nyama, ichanganye ili limao lichanganyike vizuri.
 • Ponda tangawizi kwenye kinu, iwe laini.
 • Ponda kitunguu swaumu kwenye kinu, ilainike vizuri.
 • Weka viungo - chumvi, cube maggie, tangawizi na kitunguu saumu kwenye nyama. Changanya nyama ili viungo vipate kuchanganyika vizuri. Acha nyama ikae kwa dakika 40 kwenye jokofu ili viungo viingie vizuri. Jinsi viungo vinavyokaa vizuri kwenye nyama ndio inazidi kunoga.
 • Bandika sufuria au kikaangio jikoni, weka mafuta kiasi. Subiria yapate moto.
 • Weka nyama kwenye mafuta.  Koroga ili ichanganyike vizuri na mafuta kisha funika sufuria au chungu na mfuniko. Fanya hivi ili kuiacha nyama ikaangwe na mafuta lakini inaiva na mvuke wake pia. 
 • Geuza geuza nyama kila mara ili kuzuia isigande kwenye chombo cha kupikia. Subiria hadi iive.
 • Angalia kama nyama imeiva. Unaweza kuongeza pilipili manga ya unga ili kuleta ladha tofauti kwenye nyama.
 • Ukimaliza unaweza kutenga na kula. Ni vizuri ukala kwa kachumbari nzuri pamoja na kinywaji upendacho.

MAPISHI YAPENDWAYO

Kuku wa mchuzi
dakika 25
Walaji: 4

Broccoli ya bamia
dakika 15
Walaji: 4

Toa maoni yakonoela
12:14, Fri 23 Oct 2015

nimefurahishwa sana na mapishi yenu matamu. tafadhali ningeomba kupata taarifa ya mapishi ya misosi mitamu kila mara, asanteni sana.

JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.