Nyama yenye curry sauce

Umeshakula nyama tofauti, lakini hii bado hujaionja. Viungo vilivyo kwenye nyama hii inaifanya nyama iwe laini, tamu na yenye harufu nzuri. Ni mojawapo ya vile vilivyopikwa kwa ajili ya sikukuu ya pasaka, na vilikuwa na mvuto wa kipekee.

Mahitaji

 • Nyama kilo 1
 • Pilipili mbuzi 1
 • Karoti 2
 • Pilipili hoho 1
 • Mafuta ya kula
 • Tangawizi kijiko 1½  kikubwa
 • Vitunguu maji 3
 • Vitunguu saumu 2
 • Pilipili manga kijiko 1 kikubwa
 • Chumvi
 • Majani ya rosemary kiasi
 • Curry powder kijiko 1 kikubwa
 • Soy sauce nusu kikombe cha kahawa.
 • Ndimu 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Hii nyama ni rahisi kuandaa, na matokeo yake ni mazuri. Cha muhimu ni kusoma kwa ufasaha na kufuata kila hatua ili kupata matokeo mazuri.

 • Andaa nyama. Kata vipande kisha osha vizuri. Weka kwenye sufuria safi, kamulia ndimu. Kata vitunguu maji, vitunguu saumu, weka tangawizi, pilipili manga, majani ya rosemary, mafuta, chumvi na pilipili mbuzi. Changanya zote kwenye sufuria yenye nyama. Usiongeze maji, funika sufuria vizuri na acha nyama ichemke hadi maji yakauke.
 • Maji yakikakuka funua, koroga. Kama nyama ikiwa bado inanata kwenye sufuria, ongeza maji kidogo na usiache kukoroga.
 • Nyama ikiiva kabisa weka soy sauce, kata pilipili hoho, karoti kisha weka kwenye sufuria. Weka curry powder, koroga vizuri. Hakikishash maji yameisha na yamebaki mafuta. Karoti na hoho zikiiva, epua nyama itakua tayari kuliwa.
 • Unaweza kula nyama hii na vyakula tofauti, au yenyewe kama kitafunwa cha kawaida. Ni vyema ukila na ugali.

MAPISHI YAPENDWAYO

Koni za asali
dakika 25
Walaji: 10

Wali & mboga mseto
dakika 45
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.