Nyanya chungu zilizochanganywa na bamia

Nimedokezwa kuwa mboga hii inasaidia sana kuleta ashki na kongeza stamina ya mapenzi kwa wanaume. Uwezo wake wa kuongeza stamina ni kutokana na uwepo wa vitamin K ambayo husaidia kuimarisha mishipa ya damu na kuboresha mzunguko wa damu. Damu ni kitu muhimu sana kwa mwanaume lijali. Nimeweka hapa ili wale wanaopenda wajue umuhimu wake, jaribu pia ili ujue, maana huna cha kupoteza.

Mahitaji

 • Nyanya chungu 3
 • Karoti 1
 • Bamia 4
 • Kitunguu, mie nimetumia majani ya kitunguu au leeks
 • Kinogesha mchuzi
 • Chumvi
 • Pilipili hoho 1
 • Pilipili manga
 • Mafuta ya kula, binafsi nimetumia mafuta ya zaituni (Olive oil)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Andaa kitunguu (majani ya kitunguu) na karoti kwa kumenya kisha kata vipande vidogo. Kata ncha za bamia kisha kata vipande vidogo. Hifadhi pembeni.
 • Osha nyanya chungu, usimenye wala kuzikata. Weka pembeni.
 • Bandika kikaango au sufuria jikoni. Acha kipate moto vizuri. Weka mafuta ya kula.
 • Acha yapate moto kisha weka kitunguu. Koroga vizuri hadi kilainike na kuanza kubadilika rangi. Ongeza bamia, koroga kwa dakika 2, ongeza karoti kisha koroga zaidi. Acha kwa dakika mbili kisha weka pilipili hoho, nyanya chungu. Koroga kisha funika vizuri. Acha viive.
 • Epua na kisha andaa chakula ujirambe vizuri.

misosi-bamia-nyanya-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Kabeji yenye royco
dakika 10
Walaji: 4

Samaki wenye sauce ya pilipili
dakika 35
Walaji: 4

Maandazi ya apple
dakika 5
Walaji: 5

Tambi za maziwa na iliki
dakika 15
Walaji: 3

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.