Omelette za pilipili hoho

Kwenye mapishi haya tunaandaa yai la pilipili hoho ambalo unaweza kula wakati wowote kama kitafunwa au maalum wakati wa staftahi.

Mahitaji

 • Mayai 2
 • Kitunguu saumu
 • Chumvi ½ kijiko cha chai
 • Pilipili manga
 • Kitunguu maji 1
 • Pilipili hoho 3 – ya kijani, ya njano ya nyekundu
 • Olive oil

20141207_130545

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Tukimaliza kuandaa tunapata kitu kinachofanana hivi:

20141207_132024

 • Kata pilipili hoho kwenye uviringo na upana unaoridhisha. Kisha ondoa mbegu za ndani na weka vizuri kwenye chombo pembeni.
 • Pasua mayai, koroa kiasi. Ongeza chumvi kisha koroga.

20141207_131214

 • Ongeza pilipili manga kwenye yai, kisha koroga kiasi
 • Kata kitunguu maji kwenye vipande vidogo, kisha weka kwenye chombo pembeni
 • Weka kikaangio jikoni, ongeza mafuta ya olive. Acha yapate moto kiasi
 • Weka vitunguu. Acha vipate kuiva kiasi. (Hapa sikutumia vitunguu maji, ila unaweza kuweka kama unapendelea)
 • Weka pilipili hoho kwenye kikaangio. Zipange vizuri ili zisipandiane

20141207_131115

 • Baada ya dakika kama 1, nyunyia mchanganyiko wa yai vizuri kwenye uviringo wa pilipili hoho, angalia isimwagikie pembeni.

20141207_131423

 • Acha yai liive kwa dakika 2 au 3 kabla ya kugeuza pilipili hoho. Kuwa makini, tumia chombo bapa na kikubwa katika kugeuza ili usiharibu umbo la yai.
 • Fanya hivyo kwa zote tatu
 • Baada ya dakika 2 litakuwa limeiva na kisha toa na tenga tayari kwa kula.

20141207_132024

20141207_133131

Mlo mwema :)


MAPISHI YAPENDWAYO

Mapishi ya kabeji
dakika 12
Walaji: 4

Samaki wa mchuzi wa nazi
dakika 15
Walaji: 5

Mapishi ya spinach
dakika 18
Walaji: 3

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.