Paella

Paella ni chakula chenye asili ya kispaniola (Spanish recipe). Chakula hiki hupikwa kwa mapishi tofauti yanayochanganya wali na mboga tofauti – mfano: nyama, sausage, na vyakula toka baharini. Kwenye paella hii tumetumia prawns, kuku, na mboga nyingine tofauti. Ni chakula kizuri kula na familia maana kina ladha tamu na afya kwa wingi.

Mahitaji

 • Vijiko 2 vya mafuta ya zaituni (olive oil)
 • Kijiko 1 kikubwa cha paprika
 • Vijiko 2 vidogo vya oregano kavu (Jamii ya majani ya mnanaa au mint)
 • Chumvi na pilipili
 • Kilo 1 ya minofu ya kuku, iliyokatwa kwenye vipande vidogo
 • Vijiko 2 vikubwa vya mafuta ya zaituni (olive oil), tenga pembeni kwenye chombo tofauti
 • Punje 3 za za karafuu, ponda
 • Kijiko 1 kidogo cha pilipili iliyopondwa
 • Vikombe 2 vya mchele mweupe
 • Karoti ½  kilo
 • 1 majani ya bay 
 • Italian parsley, kata vipande 
 • ¼  lita ya supu ya kuku
 • Malimao 2, kwangua majani (zest) na weka pembeni
 • Vijiko 2 vikubwa vya mafuta ya zaituni (olive oil)
 • Kitunguu 1 kikubwa, kata vipande
 • Pilipili hoho 1, kata vipande vikubwa
 • Sausage za choriz o ½ kilo , kata vipande vidogo vyembamba
 • ½ kilo ya kamba (prawns),menya maganda

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kuwa huru kuongea au kupunguza mahitaji kutokana na unavyopenda. Cha muhimu ni kula chakula unachopenda wakati unajaribu mapishi mapya.

misosi-paella

 • Kwenye bakuli ya wastani, changanya vizuri kwa pamoja vijiko 2 vikubwa vya mafuta ya zaituni (olive oil), paprika, oregano, chumvi na pilipili. Weka vipande vya kuku, changanya vizuri ili vipate kuenea mchanganyiko vizuri. Funika na weka kwenye jokofu.
 • Bandika sufuria kubwa jikoni, weka vijiko 2 vikubwa vya mafuta ya zaituni, weka moto wa wastani. Weka kitunguu saumu, pilipili, na mchele. Pika kwa kukoroga, changanya mchele na mafuta, kwa dakika takribani 3. Weka majani ya bay, parsley, supu ya kuku na maganda ya malimao yaliyokwanguliwa (lemon zest). Funika, acha vichemke kwa pamoja. Punguza moto uwe wa wastani.  Acha ikae kwa dakika 20.
 • Wakati wali unaiva, weka kikaango jikoni, weka vijiko 2 vikubwa vya mafuta ya zaituni (Olive oil)  kwenye moto wa wastani. Weka kuku alicovywa kwenye supu ya pilipili na kuhifadhiwa kwenye jokofu. Weka kitunguu; pika kwa dakika 5. Weka pilipili hoho na sausage; pika kwa dakika 5. Weka kamba (prawns); changanya kiasi, pika hadi pande zote ziwe na rangi ya pink.
 • Tandaza wali kwenye sinia au sahani. Weka nyama na mchanganyiko wa mboga tofauti – kamba (prawns).

misosi-p


MAPISHI YAPENDWAYO

Ndizi mzuzu na sauce ya ukwaju
dakika 30
Walaji: 3

Samaki wa kupaka
dakika 60
Walaji: 2

Cheese Burger
dakika 15
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.